INAELEZWA kuwa nyota wa Yanga, Bernard Morrison amemalizana
na uongozi wa Smba hivyo anaweza kutangazwa muda wwote kuanzia leo Agosti 7.
Habari
zinaeleza kuwa Morrison tayari ameshamalizana na Simba kilichobaki kwa sasa ni
kutangazwa ndani ya kikosi hicho cha Simba.
'Tayari
Simba wamemalizana na Morriosn kilichobaki ni kutanagazwa tu ndani ya kikosi
hicho," ilieleza taarifa hiyo.
Injinia
Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya GSM ambao ni wadhamini wa
Yanga amesema:"Inashangaza kwa kuwa bado Morrison ana mkataba na kesi yake
bado inaskilizwa, hivyo itakuwa ni ajabu kutangazwa leo najua kamati
inafuatilia mambo yaliyopo
"Kwa
harakaharaka nimegundua kwamba mchezaji ni wetu, nikiangalia naona picha mbaya
sana kama mchezaji atasaini na amekuwa na matatizo ya nidhamu kwa muda mrefu,
amekuwa akisema kwamba viongozi wa Simba wamekuwa wakimlaghai ili kumpa mkataba
hivyo kama atatangazwa leo basi itatoa picha kwamba Simba walikuwa nyuma katika
haya," amesema.
0 Comments