SUAMEDIA

Wafugaji wa kuku wametakiwa kuzingatia chanjo

Na:Farida Mkongwe
Wafugaji wa kuku wametakiwa kuzingatia suala la chanjo kwa mifugo
yao ili kuwaepusha kuku wao na vifo ambavyo vinaweza 
kuwasababishia kupata hasara.

Wito huo umetolewa na Afisa Kilimo kutoka Idara ya Tiba ya Mifugo na Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Bibi. Enesa Raphael Mlay wakati akizungumza na SUAMEDIA kwenye maonesho ya wakulima Nanenane mkoani Morogoro. 

Bibi Mlay amesema kuku wa asili iwapo watapewa chanjo kwa wakati
na kwa mpangilio unaokubalika basi wanaweza kumletea faida kubwa
mfugaji kwa kuwa wanauwezo wa kutaga mayai mengi na kuatamia

“Kuku wana changamoto nyingi katika ufugaji wake lakini

kikubwa ni kuzingatia chanjo hilo ndilo suala muhimu sana kwani

kuku wasipopewa chanjo wanaweza kufa wengi kwa wakati

mmoja kutegemeana na aina ya ugonjwa watakaoupata”,

amesema Bibi. Mlay

Afisa Kilimo huyo pia amewataka wafugaji wazingatie suala la utunzaji
wa mayai, usafi wa banda na utunzaji wa vifaranga kwa kuhakikisha
wanaweka katika eneo lenye joto linaloshauriwa na wataalamu wa
mifugo.


Post a Comment

0 Comments