Na:Farida Mkongwe
Jamii imeshauriwa kuacha tabia ya kunywa maziwa yasiyochemshwa
na kuacha kula nyama isiyoiva vizuri ili kuepukana na ugonjwa wa
kutupa mimba ambao ambao ni hatari kwa afya ya binadamu.

Ushauri huo umetolewa na Mtafiti kutoka Ndaki ya Tiba ya Wanyama
na Sayansi za Afya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
HILDEGALDA COLMAN wakati akizungumza na SUAMEDIA
kwenye maonesho ya Nane Nane mkoani Morogoro.

Mtafiti huyo amesema ugonjwa huo ambao kitaalam unajulikana
kama “BRUCELLOSIS” unaotoka kwa wanyama kama ng”ombe,
mbuzi na kondoo kwenda kwa binadamu pia unaambukiza kwa njia
ya hewa hivyo ni vema wafugaji wakaepuka kulala na mifugo yao
kwa nia ya kuilinda.

“Unywaji wa maziwa mabichi hata kama yamegandishwa sio salama
kwa afya zetu, ni vizuri tukachemsha lakini pia ulaji wa nyama
ambazo hazijaiva vizuri zikiwemo nyama za kuchoma ni hatari
kiafya, tujitahidi sana kuzingatia, pia tutumie mbwa kama walinzi
wa mifugo yetu badala ya kulinda wenyewe”, amesema Hildegalda.

Mtafiti huyo amesema tafiti zinaonesha kuwa ugonjwa huo ambao
unaweza kutoka kwa ng’ombe, mbuzi na kondoo pia unaweza
kumpata binadamu kwa kugusana na mnyama anayeugua ugonjwa
huo.

“Hatuwezi kujitenga au kuacha kuisaidia mifugo yetu, lakini
tunapotoa msaada mfano kumsaidia ng’ombe kuzaa basi tuchukue
tahadhari kwa kuvaa vifaa kinga na pia tuhakikishe mazingira
yanakuwa safi wakati wote’, alisistiza Mtafiti huyo kutoka SUA.

0 Comments