SUAMEDIA

Kiwango cha sukari kinachozalishwa nchini kinatosha kukidhi mahitaji - Prof. Keneth Bengesi

 Na.Vedasto George.
Imeelezwa kuwa kiwango cha  sukari kinachozalishwa nchini 
; kinatosha kukidhi mahitaji ya walaji pasipo kuagiza bidhaa hiyo
kutoa nje ya nchi kama ilivyo kuwa awali




Akizungumza na SUAMEDIA katika mahojiano maalumu kuhusu hali ya  upatikanaji wa bidhaa hiyo ya sukari nchini Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari  Prof. Kenethi Bengesi amesema viwanda vya ndani tayari vimeshaanza uzalishaji sukari na kusema kuwa changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo muhimu itakuwa historia hapa  nchini.

   “Kipindi kile ambacho kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa
sukari ni kwa sababu kila mwaka inapofika mwezi wa tatu viwanda
vya ndani huwa vinasimamisha uzalishaji kwa ajili ya kupisha matenge
nezo na kufanya maandalizi ya kuanza msimu mpya wa mavuno na hii
huwa inatokana na kipindi hicho mvua zinakuwa nyingi na mvua
zinapokuwa nyingi ukivuna muwa unakuwa hupati sukari ya kutosha,”
alisema Prof.Bengesi

Aidha Prof. Bengesi amesema serikali kupitia bodi ya sukari tayari
imeishaweka mikakati Madhubuti ya kuhakikisha sukari inakuwepo ya
kutosha nchini ikiwemo kufanya maboresho makubwa katika viwanda
vya ndani vinavyozalisha sukari vya Kagera Sugar, Mtibwa Sugar,
Kilombero Sugar pamoja na TPC.

“Lakini bodi ya sukari kupitia serikali inaandaa mazingira mazuri ya
kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwekezaji mpya, kunakuwa na
viwanda vingine vipya ambavyo vinaanzishwa  ambavyo na vyenyewe
vitazalisha sukari na vitaingia katika kapu moja ambalo litakwenda
kuondoa tatizo la upatikanaji wa sukari nchini” alisisitiza Prof.Bengesi.

Pia ameongeza kuwa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Kagera Sugar 
kilichopo mkoani Kagera tayari kimeshapata eneo kubwa la Kitengule
lenye ukubwa wa  hekta 13,000 ambazo zitalimwa zao la miwa ambapo
mpaka sasa wameshalima miwa katika eneo hilo takribani 3,000.

Pia amesema kiwanda cha Kagera sugar ifikapo mwaka 2024 na 2025
kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 100,000  ambapo kwa sasa
kiwanda kinazalisha sukari tani 90,000 pekee huku kiwanda cha
TPC kikiwa kimewekeza zaidi katika teknolojia  ambazo zitasaidia
katika uzalishaji wa miwa.

Akizungumzia ujenzi wa kiwanda kipya cha Mkurazi ambacho ujenzi
wake unatarajia kuanza hivi karibuni  amesema kitakapo kamilika
kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 50,000 huku kiwanda kipya cha 
Bagamoyo Sugar ambacho ujezi wake unaendelea hivi sasa  kitakuwa na
uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani 50,000 ongezeko hilo la miradi mipya
  likatajwa kuondoa changamoto ya upatikanaji wa sukari nchini.

Prof. Bengesi amesema katika  kipindi cha miaka mitano ijayo Tanzania
haitegemei kuwa na upungufu wa sukari tena  bali  kutakuwa na sukari
ya kutosha inayokidhi mahitaji ya ndani lakini pia kutakuwa na sukari
nyingine ya ziada ya kuweza kuuza nje ya nchi.

Amesema kipindi ambacho Tanzania ilikuwa inaagiza sukari kutoka nje
ya nchi ni kipindi ambacho uzalishaji wa sukari kwa viwanda vya ndani
ilikuwa imeshuka na kulazimika kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi ili
kuweza kukidhi mahitaji ya watumiaji.




Post a Comment

0 Comments