Na Gerald Lwomile, Simiyu
Katika kuhakikisha wafugaji wa nyuki nchini wanakuwa
na elimu bora ya ufugaji, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimesema
wataalamu watakaohitimu katika kozi mpya ya shahada inayohusu ufugaji wa nyuki
watakaokuwa na weledi wa kutosha katika fani hiyo watawafikia wafugaji wengi
ili kutoa elimu waliyonayo
Dkt. Nyambilila akiongea na waandishi wa habari hawapo kwenye picha juu ya kozi mpya zinazotolewa na SUA |
Akizungumza kutoka katika maonesho ya kilimo Nanenane
Nyakabindi mkoani Simiyu Mkurugenzi wa Kurugenzi wa Shahada za Awali kutoka SUA
Dkt. Nyambilila Auri amesema kumekuwa na changamoto nyingi kwa wafugaji wa
nyuki ambazo zinaweza kumalizwa kwa
kupata wahitimu waliobobea kwenye fani hiyo
“Kumekuwa na changamoto mbalimbali katika ufugaji wa nyuki kwa mfano kuchagua mahali pazuri pakufugia ili kuleta asali yenye ubora lakini pia tumeona kuna changamoto katika zao letu la asali hasa katika viwango vya kimataifa kwa hiyo kwa kusoma Shahada hii mpya ya Sayansi ya Ufugaji Nyuki na Utunzaji wa Rasilimali Nyuki tunaweza kutoa watalaamu wanaoweza kutatua changamoto hizo”, amesema Nyambilila
Akizungumzia kozi zingine Dkt. Nyambilila amesema kuwa
SUA pia inataka kuongeza ufanisi kwenye fani ya ugani hivyo Chuo kimeamua
kuanzisha mafunzo ya Stashahada ili watakaohitimu waende kusaidia katika
shughuli za ugani
Aidha amesema SUA pia imeanzisha mafunzo ya Astashahada
katika fani ya uwindaji na uongozaji wa watalii lakini pia watahakikisha
mafunzo yanayotolewa yanamuwezesha mhitimu kujiajiri
0 Comments