Teknolojia ya Nyuklia hutumika kuboresha mazao ya Kilimo,
Mifugo sanjari na utafutaji na uboreshaji wa rasilimali ya maji. Matumizi ya
Teknolojia hii ya Nyuklia ni mkombozi katika kutokomeza wadudu waharibifu
katika mazao yatokanayo na kilimo na mifugo, hivyo kupunguza kuenea kwa wadudu
na magonjwa, kuongeza uzalishaji wa mazao, kulinda rasilimali za ardhi na maji,
kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza uzalishaji wa mifugo.
Bw.
Ngamilo amesema Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Shirika la Kimataifa la
Nguvu za Atomiki (IAEA) wamekuwa wakipanua maarifa na kuongeza uwezo katika
eneo hili kwa zaidi ya miaka 50. Matokeo na mafanikio makubwa yanaonekana
ulimwenguni kote
Hayo
yamesemwa na Bw. Peter Ngamilo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tume ya Nguvu
za Atomiki Tanzania (TAEC) wakati akizungumza na mtandao wa Fullshangweblog
katika maonesho ya Kilimo maarufu kama NaneNane yanayoendelea kitaifa
katika viwanja vya Nyakabindi, Wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Akiongezea
Bw. Ngamilo ametoa mfano wa nchi ya Kamerun kuwa imetumia vyema Teknolojia ya
Nyuklia katika uzalishaji wa mifugo na kutokomeza wadudu waharibifu,
hivyo kudhibiti magonjwa na kupelekea wakulima kuongeza mazao yao ya
maziwa mara tatu kutoka lita 500 hadi 1500 na kutoa nyongeza ya
dola Milioni 110 katika mapato ya mkulima kwa mwaka. Pia imepunguza sana tukio
la ugonjwa wa Brusela unaoambukiza sana, ambapo ugonjwa huo unaweza kutoka kwa
wanyama hadi kwa wanadamu ambao hunywa maziwa yasiyochemshwa au kula nyama
iliyopikwa kutoka kwa wanyama walioambukizwa.
0 Comments