Na: Farida Mkongwe
Serikali ya mkoa wa Morogoro imekipongeza Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA kwakuwa wabunifu katika masuala yanayohusu kilimo hali
inayosaidia kutatua changamoto za
wakulima nchini.
Mhandisi Kalobelo amesema “SUA hakuna mfano wenu, sisi kama
serikali tunajivunia sana uwepo wa chuo hiki hapa mkoani Morogoro, mmekuwa
mfano wa kuigwa mnatumia ubunifu wenu kutafuta changamoto zinazowakabili
wakulima na kisha mnatafuta ufumbuzi, kwa hilo nawapongezeni”.
“Ubunifu wenu ni katika taaluma, sisi ambao tupo serikali ni
wadau wenu wa bidhaa mnazozalisha ambazo ni wanafunzi, sijawahi kunung’unikia
wanafunzi au wafanyakazi wanaotoka SUA, ni wazi kuwa vijana wenu mnawapika
vizuri ili ni lazima mliendeleze”, alisisitiza Katibu Tawala huyo wa mkoa wa
Morogoro.
Amesema kuwa serikali inahitaji sana kutumia elimu na kutoa
wito kwa SUA kuendelea kutoa elimu kwa vitendo ili elimu hiyo iweze kuwasaidia
wananchi na hasa wakulima huku akihimiza mahusiano mazuri baina ya SUA na
taasisi nyingine za serikali.
“ Tungetaka kuona na tunapenda kwa kweli yawepo mahusiano
ambayo yatatatua changamoto zilizopo, inashangaza kuona halmashauri zinakuwa na
changamoto ambazo nyie SUA mnayo majibu ya changamoto hizo”, alisema.
0 Comments