Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch
limeitolea mwito serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuhakikisha
uchunguzi wenye ufanisi juu ya mauaji ya wanachama wanne wa chama cha siasa cha
rais Felix Tshisekedi.
Julai 12, mwili wa Dodo Ntumba ulikutwa ukielea
katika Mto Lubumbashi, na Julai 13, miili ya Mardoche Matanda na Heritier
Mpiana, wote wakiwa na umri wa miaka 18, waliopolewa kutoka mtoni.
Agosti 3, familia ya Danny Kalmbayi mwenye umri
wa miaka 29, iliukuta mwili wake katika chumba cha maiti, mwezi mmoja tangu
walipomuona kwa mara ya mwisho.
Watu walioshuhudia waliliambia shirika la Huma
Rights Watch kwamba miili yote ilikuwa na alama za kukatwa na kuondolewa
viungo, ambazo zinaweza kuwa zilitokana na mateso.
Kwa mujibu wa Human Rights Watch, vifo hivyo
vilitokea katika muktadha wa ukandamizaji unaozidi tangu mwanzoni mwa mwaka
huu.
Shirika hilo limeitaka serikali kuchunguza
taarifa kwamba marehemu hao walikuwa wanashikiliwa katika kituo cha kijeshi
mjini Lubumbashi, kufuatia maadamano ya Julai 9.
0 Comments