SUAMEDIA

Wakazi wa Kitongoji cha Kibao cha Ranchi Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero waiomba Serikali kusajiri eneo lao kuwa Kijiji

Na: Vedasto George

Wakazi wa Kitongoji cha Kitongoji cha Kibao cha Ranchi Halmashauri
ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuanga
lia uwezekano wa kusajili eneo hilo kuwa kijiji ili waweze kujitegemea.




Wakazi hao wametoa ombi hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero
Albinus Mgonya wakati wa kupokea Madawati 45 yaliyotolewa na 
Ushirika wa Vijana Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
SUGECO, kwa ajili ya Shule Shikizi ya Msingi Mtakuja Bwawani
iliyojengwa na wahisani kwa ushirikiano na wananchi.


Wakazi hao wanaoishi eneo la Bwawa la Kihonda Kitongoji cha Kibao
cha Ranchi wamedai kuwa pamoja na uwepo wa kaya zaidi ya elfu
tatu hakuna huduma muhimu za kijamii wakilazimika kufuata
huduma umbali wa zaidi ya kilomita 20.



Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Shikizi Betrice Masawe  amesema kwa
sasa kuna walimu  saba wakujitolea na changamoto iliyopo ni umbali
kutoka eneo hilo hadi ilipo shule mama ya Wami Sokoine ambako
wanafunzi wa darasa la nne na saba hulazimika kuhamia huko kipindi
cha mitihani ya kitaifa.


Mpaka sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 225 kuanzia awali
mpaka darasa la saba, ikiwa na vyumba vitatu vya madarasa ambapo
ni darasa moja pekee lililo ezekwa.









Post a Comment

0 Comments