Idadi ya maambukizi
ya virusi vya corona barani Afrika imezidi milioni moja, kwa mujibu wa takwimu
za chuo kikuu cha Johns Hopkins, lakini bara hilo linaonekana kuwa na mlipuko
mkubwa zaidi .
Nusu ya maambukizi
yanatoka katika nchi moja tu, Afrika Kusini.
Kuna kiwango kidogo
cha upimaji katika nchi nyingi, hii inamaanisha, idadi ya maambukizi inaweza
kuwa juu zaidi inavyoripotiwa.
Kwa sasa kesi nyingi
zinatokea maeneo ya miji mikubwa.
Zaidi ya watu milioni
18.6 wameripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona duniani kote na vifo
vilivyosababishwa na mlipuko huo ni 702,000, kwa mujibu wa
Shirika la Afya duniani(WHO).
Barani Afrka, watu
karibu 21,000 wamefariki kutokana na corona na watu 670,000 wamepona.
Mkurugenzi wa kituo
cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC, John Nkengasong, ameiambia BBC kuwa
asilimia sabini ya watu wenye maambukizi ya corona barani Afrika wamepona.
"Nadhani tusitaharuki
bali tuzingatie kufanya jambo sahihi na kutumia sayansi ili kukabiliana na
janga hili," alisema.
Awali Shirika la Afya
duniani lilieleza kuwa bara hili lina upungufu wa mashine za kupumulia ili
kukabiliana na mlipuko huu.
Wafanyakazi wa afya katika
maeneo mbalimbali barani humu wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa vifaa kinga vya
kuwalinda na corona wakati wakiwa kazini..
0 Comments