Na
Gerald Lwomile
Simiyu
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kinatarajia
kuanzisha kozi mpya za Kilimo na Huduma za Kibenki na kozi ya Stashahada ya Teknolojia
na Uzalishaji wa Mbegu ili kuhakikisha inawasaidia wananchi na hasa katika kusimamia
fedha zitokanazo na mikopo
Akizungumza katika maonesho ya kilimo ya Nanenane
yanayofanyika kitaifa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu Naibu Makamu wa Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Taaaluma Prof. Maulid Mwatawala amesema kozi
hiyo ina lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na watalaamu ambao watawasaidia
wakulima kujisimamia katika mikopo
Amesema kutokana na wananchi wengi kukosa uelewa juu
ya matumizi ya fedha za mikopo hali hiyo inawezekana inasababisha taasisi za
kifedha ikiwemo benki kushindwa kutoka mikopo mikubwa
“Kwa hiyo tuna uhakika kwamba hawa wataalamu watakuwa
na uwezo mzuri wa kusimamia mikopo au uwekezaji mahususi kwenye kilimo ambao
unaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kama moto, mafuriko au mabadiliko
ya tabia nchi na changamoto zingine”, amesema Prof. Mwatawala
Amesema inawezekana pia benki nyingi hazina watalaamu
wa aina hii na hii itakuwa fursa pia ya kuhakikisha wanakuwa na watalaamu
waliobobea katika fani hiyo jambo litakalomsaidia mkulima wa Tanzania
Maonesho ya Nanenane yanaendelea mkoani Simiyu na Agosti
3, 2020 Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa atakuwa mgeni
rasmi katika maonesho hayo yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu
0 Comments