Posts

Showing posts from November, 2023

Matumizi ya Akili Bandia kuboresha kilimo nchini.

Image
  Na, Winfrida Nicolaus Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Mradi wa Mkulima GPT chini ya ufadhili wa ‘BILL na MELINDA GATES Foundation’ imetoa mafunzo kwa wakulima wadogowadogo wapatao   20 mkoani Morogoro kuhusiana na Mfumo wa Akili Bandia unaotumia lugha ya kiswahili utakaomsaidia mkulima kuweza kupata ushauri kuhusiana na kilimo cha Mahindi kwa wakati husika lakini pia kutatua tatizo kwenye shamba lake bila uwepo wa Afisa Ugani. Kiongozi wa Mradi huo na Mhadhiri Msaidizi SUA kutoka Idara ya Infomatikia na Teknolojia ya Habari Bi.Theofrida Maginga akizungumza na wakulima na wadau wa kilimo Amebainisha hayo Kiongozi wa Mradi huo na Mhadhiri Msaidizi SUA kutoka Idara ya Infomatikia na Teknolojia ya Habari Bi.Theofrida Maginga wakati akizungumza na SUAMEDIA kwenye warsha iliyofanyika katika Hoteli ya Morena iliyoko Msamvu mjini Morogoro ambapo amesema Mkulima GPT ni ‘ Chatbot’ inayowasaidia wakulima kupata taarifa ya namna ya kuandaa mashamba vilevile kusimamia...

Mhe. Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba awatunuku Wahitimu 3095 katika Mahafali ya 42 SUA

Image
  Na, Winfrida Nicolaus Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimefanya Mahafali yake ya 42 ambapo Wahitimu  3 , 095 kutoka programu 74 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu  elimu yao ya Chuo Kikuu ambapo  jumla ya watunukiwa wanawake ni 1 , 360 sawa na asilimia 43.9 ya Wahitimu wote na wanaume wakiwa 1 , 735 huku wakihudhurishwa kwa mara ya kwanza Wahitimu wa kwanza wa Ngazi ya Shahada kutoka Kampasi ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi . Amebainisha hayo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda wakati akitaja takwimu za Wahitimu katika Mahafali hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Michezo vya Kampasi Kuu ya Edward Moringe ambayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Chuo hicho Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba . Katika takwimu hizo wahitimu 2 , 811 ni kutoka Shahada za Awali ambapo wanaume ni 1 , 574 na wanawake 1 , 237, Shahada za Umahiri wahitimu 56 wanaume 29, na wanawake 27, Stashahada ya Juu ya Elimu wahitimu 2 wote wakiwa ni wanaume, Shahada za Uz...

Fanyeni kazi kwa maslahi ya Taasisi - Prof. Mahonge

Image
  Na Gerald Lwomile Watumishi wa ngazi zote katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametakiwa kufanyakazi kwa maslahi ya Taasisi kwani maendeleo ya nchi na mahitaji yao kiuchumi yanategemea uwepo wa Taasisi hiyo. Prof. Christopher Mahonge akitoa mada katika semina (Picha zote na Gerald Lwomile) Akizungumza na watumishi wa Kampasi ya Mazumbai iliyopo mkoani Tanga Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu (KKU – SUA) Prof. Christopher Mahonge amesema ili nchi iwe na maendeleo inahitaji kuwa na watumishi wanaojituma katika kazi kwa kuzingatia uadilifu na kuepuka rushwa. Amesema ni vyema watumishi wakajua na kufahamu utawala bora ambao umebeba mambo mengi ikiwa ni pamoja na uadilifu, uwajibikaji, uwazi, utawala wa sheria, haki bila upendeleo, ushirikishwaji na kuepuka rushwa. Prof. Christopher Mahonge aliyekaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumushi wa Kampasi Mazumbai aliyekaa (kushoto) ni Meneja wa Kampasi ya Mazumbai Bw. Steven Kingazi na kulia ni Lightness...

Tafiti SUA zinaisadia Serikali uwekezaji kilimo- Katibu Tawala Iringa

Image
Na Gerald Lwomile Jitihada za Serikali katika kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo na mazingira ya uwekezaji katika sekta hiyo, kumepelekea Tanzania kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika sekta ya kilimo katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bw. Elias Luvanga aliyekaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofikia katika kupata mrejesho wa utafiti, kulia waliokaa ni Prof. Karimuribo na kushoto ni Dkt.  Helle Ravnborg (Picha na Gerald Lwomile) Akizungumza mkoani Iringa katika siku ya kuwasilisha matokeo ya utafiti wa ‘Wawekezaji wa Kilimo ni wadau wa Maendeleo?’ (AIDA), Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bw. Elias Luvanda amesema utafiti huo una manufaa makubwa kwa nchi ya Tanzania. Amesema utafiti huo uliofanyika pamoja na kuwa na matokeo chanya katika baadhi ya maeneo, utaisadia Serikali kuboresha na kuhuisha Sera, Sheria na Miongozo yake iwe rafiki kwa wawekezaji na wadau wa kilimo ili kuakisi uhalisia kwenye m...

Miradi ya Tafiti inahitaji ushirikiano katika kuongeza Tija na Uzalishaji wa Tafiti zenye ubora- Prof. Kashaigili

Image
Na, Winfrida Nicolaus Utekelezaji wa Miradi ya Utafiti  inayohitaji utaalam ni muhimu ikaandikwa kwa ushirikiano baina ya watafiti mbalimbali wakiwemo wa ndani na nje  ya nchi  ili kuongeza Tija na uwezekano wa kupata ufadhili zaidi ya hayo ni  kufanya Tafiti zitakazo zalisha matokeo bora. Prof. Japhet Kashaigili  M shindi wa Tuzo ya Mtafiti bora wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa mwaka 2022/2023   akipokea Cheti cha Ushindi kutoka kwa  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Carolyne Nombo. Hayo yameelezwa na Prof. Japhet Kashaigili ambae ni Mratibu wa Utafiti na Machapisho kutoka Chuo Kikuu c ha Sokoine c ha Kilimo ( SUA )  na Mshindi wa zawadi ya Mtafiti bora wa Chuo kwa mwaka 2022/2023 wakati akizungumza na SUAMEDIA kwenye   M kutano  wa Majalisi SUA ambao uliambatana na utoaji wa T uzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao na  watafiti katika Tafiti na kukiletea tija C huo  hicho . Prof. Kashaigili  a...