Na Gerald Lwomile
Simiyu
Serikali imewataka vijana kuingia katika kilimo kwani sekta
hiyo ina fursa nyingi ikiwa ni pamoja na ajira, kupata mikopo na chakula cha
uhakika kwa kaya na taifa
Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wa pili kutoka kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wa tatu kutoka kulia
Akitembelea maonyesho ya nanenane Agosti 2, 2020 katika
viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Antony
Mavunde amesema endapo vijana wataamua kuingia katika kilimo biashara kinaweza
kuwatoa kiuchumi na kuinua maisha yao
Amesema wakati sasa umefika wa kutekeleza mipango
waliojiwekea katika kuwasaidia vijana ili wajiingize katika kilimo chenye
uhakika wa kupata masoko
Mhe. Mavunde amewataka watendaji wa program ya
kuendeleza Sekta ya Kilimo ya Pili ASDP 2 kutekeleza mpango wa kuwasaidia
vijana katika sekta ya kilimo
0 Comments