Wakati
wanafunzi wakitegemea kuanza rasmi muhula wa masomo katika Kampasi mpya ya Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Kampasi ya Mizengopinda Katavi, chuo
kimeendelea kuhakikisha miundombinu yote inakamilika kwa wakati.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amefanya ziara katika kampasi hiyo ili
kuhakikisha miundombinu yote imekamilika kwa wakati na kuwa rafiki kwa
wanafunzi wapya watakaoanza masomo yao November 11 2020.
Chibunda akiwa kwenye ziara hiyo amekagua maeneo yote na kujionea
maandalizi yakiendelea kwenye Ufungaji wa Vitanda kwenye mabweni, Viti kwenye
madarasa, Miundimbinu ya Maji na Umeme kwenye kampasi yote, na marekebisho
mengine muhimu ili wanafunzi watakapofika kuwapo chuoni hapo na hivyo kusoma
vizuri.
Makamu huyo amesema
siku ya ijumaa agost 29, 2020 Kampasi hiyo itatembelewa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Mdoe ambaye atafikia kuona
mazingira na namna Chuo hicho kilivyojipanga kutoa elimu na kusaidia jamii ya
Mikoa inayopakana cha Kampasi hiyo.
Aidha amebainisha kuwa Kampasi ya Mizengo Pinda itaanza kutoa
mafunzo ya kozi tatu ambazo ni Ashashada ya Utalii na Uongozaji Watalii,
Stashahada ya Kilimo na Shahada ya Nyuki na mazao ya nyuki.
Nae Mkuu wa Kampasi hiyo Prof. Mwamengele
amesema maandalizi yapo kwenye hatua za mwisho na wanamalizia kufanya kazi
ndogondogo ambayo ndani ya wiki chache yatakuwa yamekamilika.
Pia ametoa wito kwa jamii na wahitimu wa kidato cha nne, cha
sita, na wale wenye astashahada na stashahada wenye nia ya kujiunga na vyuo vya
elimu ya juu kuchagua Kampasi ya Katavi kwakuwa ina miundombinu mizuri kwa
wanafunzi kusoma na kufanya Mafunzo kwa vitendo kwenye kozi ambazo zitatolewa
Chuoni hapo.
0 Comments