Posts

Showing posts from November, 2025

SUA yawajengea watumishi uwezo wa udhibiti vihatarishi kupitia mafunzo

Image
  Na: Ngolo Mboje Watumishi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wamepatiwa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo katika kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utendaji wa taasisi, kufuatia mwongozo wa Serikali wa mwaka 2023 kuhusu usimamizi wa vihatarishi katika taasisi za umma. Mafunzo hayo yametolewa tarehe 21 Novemba, 2025 katika Kampasi ya Edward Moring e mjini Morogoro, yakilenga kuongeza uelewa, umahiri na uwezo wa watumishi katika kutambua, kuchambua na kudhibiti vihatarishi kwenye idara zao. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Bariki Mtunha , amesema Serikali imeweka msisitizo kwa taasisi za umma kuimarisha mifumo ya udhibiti wa vihatarishi ili kuboresha uwajibikaji na ufanisi wa taasisi. Amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwasaidia watumishi wa SUA kupata uelewa mpana juu ya namna ya kusimamia masuala ya vihatarishi kwa ufanisi zaidi. Mtunha ameongeza kuwa SUA imeonesha mafanikio makubwa katika kuimarisha mi...

Ufugaji wa kuku una mchango katika kuondoa umaskini

Image
  Na: Vumilia Kondo Mafunzo ya ufugaji bora wa kuku kwa wafugaji 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini, yamemalizika Novemba 20   katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, yakilenga kuongeza uzalishaji wa mayai na nyama pamoja na kuboresha lishe ya jamii. Afisa Tawala wilaya ya Morogoro Bw. Hilary Sagala waliokaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakulina na wataalamu. wa pili kutoka (kushoto) ni  Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. Agnes Sirima Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagala ambaye ni Afisa Tawala   amesema ufugaji bora wa kuku una mchango mkubwa katika kupunguza umasikini Amesema watumishi wengi na wafanyakazi wa sekta binafsi wanapaswa kupata nafasi ya kujifunza ili hata wanapostaafu waweze kuwa na shughuli za kukuza uchumi wao na kupunguza umaskini katika Kaya. Kwa upande wake, mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ambaye ni Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na...

SUA kupitia Mradi wa SANIRICE kutumia teknolojia ya kidijitali na akili mnemba katika uzalishaji wa Mpunga.

Image
Na: Gerald Lwomile Imeelezwa kuwa kutokana na umuhimu wa zao la mpunga kibiashara na chakula, uzalishaji wake umeambatana na matumizi holela ya mbolea hasa aina ya naitrogen ambapo kiasi kinachozidi huchangia uchafuzi wa maii na kuongeza gesi chafuzi aina ya nitrous oxide kwenye anga la dunia. Profesa Mshiriki na Kaimu Mratibu wa Masomo ya Umahiri na Uzamivu Prof. Akwilina Mwanri wa pili kutoka kulia mstali wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mradi wa SUNIRICE Hayo yamesemwa na Profesa Mshiriki na Kaimu Mratibu wa Masomo ya Umahiri na Uzamivu Prof. Akwilina Mwanri wakati akizindua mradi wa SANIRICE ambao utafanywa Tanzania Bara. Profesa Mshiriki na Kaimu Mratibu wa Masomo ya Umahiri na Uzamivu Prof. Akwilina Mwanri akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa SANIRICE Prof. Akwilina amesema utafiti utakaofanywa na mradi huo utasaidia kupunguza matumizi holela ya mbolea ili kuthibiti kiwango cha ges chafusi na kuwa kilimo endelevu cha mpunga.. Amesema Chuo Kikuu cha Sok...

SUA yawapa elimu na pongezi wanafunzi wa mwaka kwanza 2025/2026

Image
  Na: Ngolo Mboje Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Uhamiaji mkoani Morogoro, kimetoa elimu na kuwapongeza wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliojiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine, November 17 2025 Kaimu Mkuu wa   Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo ( SUA) Bi. Suzan Magobeko, amewaapongeza wanafunzi hao na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa chuo, hususan kupitia mitandao ya kijamii. Aidha, Kaimu Mkuu Mlezi wa Idara ya Ushauri kwa Wanafunzi SUA, Bi. Hilda Gamuya, amesema kuwa mwitikio wa wanafunzi wa mwaka huu ni mzuri tofauti na mwaka wa masomo 2024/2025, kwani wana imani kuwa elimu wanayoitoa inaweza kuleta hamasa na mtazamo chanya ili kuendana na utaratibu wa chuo. Bi. Hilda ameongeza kuwa matarajio yao makubwa ni kuona wanafunzi wanabadilika na kuendana na utaratibu, sheria na kan...