Na Gerald Lwomile
Simiyu
Serikali imesema sasa ina uhakika kuwa wafugaji wengi
watanufaika na ubunifu mpya wa namna ya kuhifadhi chanjo katika maeneo ambayo
hayana umeme, ubunifu uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisikiliza maelezo kutoka kwa Prof. Ludovick Kazwala
Akizungumza na SUA Media mara baada ya kutembelea banda
la maonesho la Chuo hicho katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema kwa muda mrefu kumekuwa na
shida ya kuhifadhi chanjo katika maeneo ya vijijini lakini kwa kutumia ubunifu
sasa wafugaji watapata huduma kwa wakati
“Tumeona ubunifu mpya wa kuhifadhi chanjo kwenye chombo kinachotengenezwa ambacho kwa vyovyote vile kina bei ya chini sana kuliko vile vifaa vingine ambavyo vinajumuisha mitungi ya gesi na wakati mwingine matengenezo makubwa…..., si kila eneo la wafugaji linakuwa na umeme hivyo hii itasaidia sana”, amesema Waziri Mpina
Awali akitoa maelezo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Prof. Ludovick Kazwala amesema katika kuhakikisha wafugaji wananufaika na
ubunifu huo watahakikisha wanashirikiana na serikali katika kuangalia uwezekano
wa kusambaza ubunifu huo
Katika hatua nyingine serikali imeagiza kuwepo kwa
ushirikiano wa mambo ya utafiti kati Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na
Taasisi ya Utafiti Kilimo Tanzania TARI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa miche ya matunda
Akizungumza katika banda la SUA Naibu Waziri wa Kilimo
Mh.Hussein Bashe amesema kuwa kama SUA na TARI zitafanya kazi kwa kushirikiana
anaona kutakuiwa na maendeleo makubwa ya kilimo nchini
Aidha Mh. Bashe amekishukuru Chuo Kikuu ca Sokoine cha
Kilimo SUA kwa kukubali maabara zake kutumika katika kuongeza thamani ya mazao
ya mbogamboga
0 Comments