Serikali kuwasilisha Rasimu ya Taarifa ya Hali ya Haki za Binadamu
Na Vumilia Kondo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeingia katika hatua ya lala salama ya kuhakiki Rasimu ya Taarifa ya Hali ya Haki za Binadamu nchini (UPR), itakayowasilishwa mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Zainab Katimba akizungumza katika mkutano Akifungua kikao kazi cha uhakiki wa rasimu hiyo mkoani Morogoro, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Zainab Katimba amebainisha kuwa mchakato huo ni kielelezo cha utashi wa kisiasa wa Tanzania katika kuheshimu utu na misingi ya kisheria. Naibu Waziri ameeleza kuwa katika mzunguko wa tatu uliopita, Tanzania ilikubali kutekeleza jumla ya mapendekezo 187, jambo ambalo ameliita kuwa ni ahadi ya kitaifa na kielelezo cha utayari wa nchi katika kujitathmini. "Taarifa mnayoandaa si taarifa ya kawaida, ni taswira halisi ya namna Serikali inavyotekeleza wajibu wake, uimara wa taasisi zetu na athari za kazi zetu katika maisha ya wananchi."Amese...