Na.Vedasto George.
Hatimaye wananchi Elfu tano wa Vijiji vya Makuyu na Chiwanga kata ya Itaragwe Wilayani Gairo Mkoani Morogoro wameanza kunufaika na Mradi wa maji uliotekelezwa na Wakala wa maji vijijini RUWASA Chini ya mkandarasi Chakwale Copany LTD kwa kiasi cha Zaidi ya shilingi milioni miasiba ambaye amejenga tanki la lita laki moja ambalo litaudumia vijiji ivyo ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Wakizungumza katika uzinduzi wa mradi huo Heleni Michael, Claudia Daniel na Agines Mataja wananchi wa vijiji ivyo wamesema kwa kipindi cha Zaidi ya miaka mitano sasa wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji safi na salama kutoka katika mabwawa yaliyapo kijijini hapo ambayo maji si safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
''Tunamshukuru Raisi wetu Magufuli ametusaidia sana kwa kipindi cha nyuma tulikuwa tunapatashida maji tunafuata mabondeni yanapatikana kwa shida tunakuta foleni hadi mnagombana lakini sasa ivi tunapata maji nyumbani kwa kweli tunamshukuru sana tunafurahi wananchi tuna amani mungu ambariki sana Raisi wetu kwa kipindi hiki cha miaka mitano ametufanyia mambo mazuri sana hatuwezi kumsahau.
Sisi wanawake katika kata hii ya Iyogwe na Itaragwe tunamshukuru Raisi wetu magufuli kwa tendi hili la kutuletea maji safi na salama ambapo kipindi kilichopita miaka yote ulikuwa tunatumia maji ya bondeni ambayo sio salama sana kwa mwananchi sasaivi maji ndi kama haya yanatoka unayapata maeneo ya karibu tunatumia muda wa dakika tatu hadi nne kupata maji walisema wanakijiji hayo.
Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa maradi huo na hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Vijiji vya Makuyu na Chiwanga Mozes Msuya Meneja Wakala wa maji vijijini UWASA Halmashauri ya Wilaya ya Gairo amesema ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lenye ukubwa lita za ujazo lakimoja tayali limekamilika huku vituo kumi na saba vya kuchotea maji vimejengwa katika vijiji ivyo na kukamilika kwa asilimia miamoja.
''Mradi huu unajumuisha vitu vifuatavyo kulikuwa na ujenzi wa tenki la kuifadhia maji la lita laki moja ambalo amelitembelea leo limekamilika, hali ya maji katika Vijiji vya Makuyu na Chiwanga kabla ya mradi huu wananchi wengi wanafahamu walikuwa na visima vya HAND PUMP vilivyo kuwa kwenye mabonde kule ambako wananchiwengi walikuwa wanakwenda kule kwenye visima wanachota maji wanakuja huku lakini kwa saizi wananchi wote wanasubiri maji kupitia bomba ambazo tumeisha hanza kufanya majaribio ya mradi huu Alisema Mozes Msuya Meneja Wakala wa maji vijijini RUWASA Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mkuu wa Wilaya hiyo Siriel Nchembe akatoa salamu za serikali na kusema kuwa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni kumi nambili zimeisha tolewa na serikali kuu kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiweo miradi ya maji.
''Serikali ya awamu ya tano ili haidi kumtua mwanamama ndoo kichwani upande wa vijijini upatikanaji wa maji safi na salama ukisoma kile kitabu cha ilani ya chama cha mapinduzi CCM ambayo inamaliza muda wake sasa upatikanaji wa maji ulitakiwa kuwa asilimia themanini na tano, naupande wa maji vijijini ni asilimia 80 na upande wa upatikanaji wa maji mjini ni asilimia 95 , sasa niwape taarifa kwa kipindi hiki cha miaka mitano nini serikali imefanya, Ngudu wananchi wa Makuyu maji mjini Gairo wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani upatikanaji wa maji safi na salama ulikuwa
asilimia 32 ndugu wananchi ninayofuraha kuwaambia leo tunapotoa takwimu hizi tuamshukuru mungu tumefikisha asilimia 70 makuyu oyeee Alisema Siriel Nchembe Mkuu wa Wilaya Gairo.
Aidha Mkuu huyo wa Wlaya amesema katika kipindi cha wikii hii ambayo anatambulika kwa Kaulimbiu maalumua ya MAGUFULI HAMTUA MAMA NDOO KICHWANI GAIRO atatembelea miradi ya maendeleo ya maji mitano ikiwemo mradi uliopo katika Kijiji cha Chogoali wenyethamani ya Zaidi ya shilingi milioni miatano,maradio wa maji Kijiji cha italagwe wenyethamani Zaidi ya shilingi milioni miatisa,mradi wa maji
Makuyu na Chiwanga wenye thamani zaidi ya shilingi milioni miasaba, mradi wa maji Kijiji cha nguyami wenyethamani Zaidi ya shilingi milioni miatatu na mradi wa maji Kijiji cha mkalama na Meshugi wenyethamani zadi ya shilingi milioni miambili.
0 Comments