Gerald
Lwomile, Simiyu
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu
wamesema tafiti zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ni za
kushangaza na zenye manufaa kwa wakulima na watanzania kwa ujumla
Wanafunzi kutoka shule ya msingi Nyakabindi wakisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Mgode wa pili kushoto |
Wakizungumza na SUAMedia kwenye viwanja vya maonesho ya
wakulima Nanenane mkoani Simiyu, Kaka Mkuu wa Shule hiyo Kulwa Kubala na Dada
Mkuu wa shule hiyo Marietha Masunga wamesema wameshangazwa na uwezo wa panya
katika kusaidia zoezi la kutambua sehemu ambayo ina bomu ili liteguliwe lakini
pia panya wanavyotumika kunasa na kutambua makohozi yenye vimelea vya Kifua
Kikuu
Akifafanua zaidi Kubala
amesema katika hali ya kawaida wakulima wengi hawajui kuwa panya wanaweza kuwa
na uwezo wa kufanya mambo hayo na wanachojua ni kuwa panya wao ni waharibifu tu
na hasa kwa kula mazao mbalimbali kama mahindi yakiwa yanaota au mpunga
unapokuwa shambani
“Nimepata mafunzo ya namna panya wanavyoweza kutumika katika kutambua na kujua wapi bomu lipo ili liondolewe lakini pia nimejifunza namna ambavyo unaweza kutumia panya kutambua makohozi yenye vimelea vya Kifua Kikuu”, amesema Kubala
Akitoa maeelezo kwa wanafunzi hao waliofika katika banda la
SUA Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Dkt. Georgies Mgode
amesema pamoja na kuwepo kwa faida za panya kutumika kama kitoweo, kutambua eneo
ambalo linakuwa na bomu na kutambua makohozi yenye vimelea vya kifua kikuu
lakini pia kuna jamii za panya ambao ni waharibifu
“Kuna aina ya panya ambao ni waharibifu ambao panya mmoja tu anaweza kula gramu 8 hadi kumi kwa siku kwa hiyo mwaka una siku 365 ukizidisha mara kumi maana yake atakula zaidi ya gramu 300, maana yake ni kwamba panya mmoja mdogo yule anaweza kula kilo 3.5 sasa wakiwa 100 je? Na ndiyo maana tunasema kuwa panya ni waharibifu pamoja na faida zake” amesema Dkt. Mgode
Dkt. Georgies Mgode mtafiti kutokaJina sahihi ni 'Kituo Cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu' SUA akitoa maeelezo kwa wanafunzi
|
Ameongeza kuwa sababu kubwa za panya kuzaliana kwa wingi ni
pamoja na kuwepo kwa nafasi nzuri, chakula na mazingira mazuri na huzaliwa hadi
panya 24 kwa mpigo na watoto katika siku 28 tu wanakuwa wamemaliza kunyonya
mama yao anazaa wengine……, sasa wanapozaliana kwa wingi wanaharibu mazao”
amesema Dkt. Mgode
0 Comments