SUAMEDIA

Wakulima na wafugaji wametakiwa kujifunza namna bora ya uhifadhi wa malisho ya mifugo

Na:Farida Mkongwe
Wakulima na wafugaji wametakiwa kujifunza namna bora ya uhifadhi
wa malisho ya mifugo kwa kutumia teknolojia zilizo rahisi ili wakati
wa kiangazi mifugo yao isipate shida ya chakula.

Wito huo umetolewa na Bw. Richard Mkama kutoka Idara ya Sayansi
ya Wanyama ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati
akizungumza na SUAMEDIA kuhusu njia bora za kuhifadhi majani
yanayotumika kwa ajili ya malisho.

Bw. Mkama amesema suala la malisho limekuwa ni changamoto
kubwa sana hasa wakati wa kiangazi hali inayopelekea mifugo
mingine wakiwemo ng'ombe kukosa lishe bora na kupoteza
virutubisho wanavyotakiwa kuwa navyo na hivyo kuwa hasara kwa
mfugaji.

“Wakati wa mvua hakuna tatizo majani yanakuwa mengi kila

kona inakuwa ni neema kwa wafugaji, tatizo linakuja unapofika

wakati wa kiangazi ambapo majani yanakuwa yamekauka,

unakuta mbavu za ng’ombe zinahesabika kutoka na kukosa

malisho ya kutosha”, amesema Bw. Mkama.

Amesema Idara ya Sayansi ya Wanyama iliyopo SUA inatoa mafunzo
kwa wakulima ya namna ya kuboresha malisho ya wanyama hivyo ni
nafasi yao wakulima kuitumia idara hiyo ili waweze kufuga kwa tija.




Post a Comment

0 Comments