Tatizo la kukosa uadilifu linaweza kuleta madhara kiuchumi na kijamii – Prof. Chibunda
Na.Gerald Lwomile Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amesema tatizo la uadilifu katika sehemu za kazi ni kubwa jambo linaloweza kuleta madhara makubwa kiuchumi na kijamii. Prof. Chibunda amesema hayo Julai 22, 2021 wakati akifungua Mafunzo ya Maadili kwa wafanyakazi wapya wa SUA, ambayo yamelenga kuwapa uelewa wafanyakazi hao juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili kazini. Prof. Chibunda akizungumza na wafanyakazi wapya wa SUA. Amesema kuwa kuna baadhi ya watumishi wamekuwa wakishiriki katika ubadhirifu wa mali za umma, rushwa na hata wizi wa vifaa mbalimbali vya kutolea huduma katika maeneo ya kazi na kukwamisha utendaji wa kazi katika maeneo mbalimbali. “Unakuta Mhudumu ambaye anatembea na mafaili ya ofisi anatoa siri za ofisi ikiwa ni pamoja na kutoa nakala na kuanza kusambaza nje na kwenye mitandao ya kijamii” amesema Prof. Chibunda. Akizungumzia kuhusu tahadhari ya ugonjwa wa COVID 19, Prof. Chibunda amesema tayari S...