Akikabidhi
mifuko hiyo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa niaba ya kamati ya ujenzi, Makamu
wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda amesema chuo
kimeguswa
na hali iliyopo shuleni hapo mara baada ya kuona wanafunzi wanasomea chini ya
miti.
‘’Chuo
kikuu hatuwezi kupata wanafunzi kama hawa wanafunzi hawajapita shule ya msingi
utakuwa ni muujiza kwa hiyo tukadhani hilo siyo tatizo la wananchi wa
Mlali
na sisi ni tatizo la kwetu, na tulichukua ni tatizo la kwetu kwanza kwa kutambua
kazi kubwa inayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais
wetu mpendwa John Pombe Magufuli ”, alisema Prof Chibunda.
Prof.
Chidunda ameongeza kuwa serikali imekuwa kifanya jitihada za dhati ili kuboresha
majengo ya shule za msingi, sekondari na vyuo lengo likiwa ni kuweka mazingira
bora kwa walimu kuweza kuwafundisha wanafunzi.
Aidha
ameitaka kamati ya ujezi wa shule hiyo ya msingi Mlali kuhakikishainasimamia
vyema matumizi ya saruji hiyo ili iweze kutumika kama ilivyo pangwana
kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika kwa wakati ili wanafunzi wapate mahala
pa kujifunzia.
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo Walimu Mkuu wa shule hiyo Omary Kibukila
amekishukuru Chuo cha SUA kwa kutoa msaada huo na kusema shule hiyo inakabiliwa
na upungufu wa madarasa 35 kati 43 yanayohitajika huku
upungufu
wa matundu ya vyoo ukiwa ni matundu 35 kati ya 41 kwa wavulana na upande wa
wasichana upungufu ukiwa ni matundu 51 kati ya 60 yanayohitajika.
Kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Mlali Mwl. Ally Mbaraka amesema halmashauri ya wilaya hiyo imeshaweka mpango wa kujenga vyumba vya madarasa tisa ifikapo mwezi wa 11 mwaka huu huku serikali kuu ikiwa tayari imetoa kiasi cha shilingi milioni 40 ambazo zitatumia kukamilisha ujezi wa madarasa pamoja na kuweka Madawati.
0 Comments