Na Samirah Yusuph
Chuo kikuu Cha dar es salaaam, kimekuja na teknolojia mpya ambazo zimelenga kuwanufaisha wakulima pamoja na kuwapunguzia adha wanazokutana nazo katika shughuli zao.
Teknolojia hizo zimeonyeshwa katika maonyesho ya nane nane yanayoendelea kitaifa katika mkoa wa Simiyu, ambapo watalamu hao wameonyesha namna ambavyo wamekuja na mbinu mpya ili kuwasaidia wakulima na wavuvi.
Akionyesha mfumo mpya wa manunuzi na uuzaji was samaki kwa njia ya mtandao Ester Mhamila mwanafunzi wa viumbe maji na uvuvi alisema, kuwa kwa kutambua adha wanazozipata wavuvi Katia kuuza bidhaa zao sokoni wameamua kuwarauisishia huduma.
"Tumeanzisha program ya fishgenge ambayo wavuvi wataitumia kuuza samaki na wanunuzi kununua samaki kwa Bei inayohitajika eleweka kupitia Application inayopatika katika simu za mkonono," alisema.
Aliongeza kuwa mbali na kufanya manunuzi vile vile mnunuzi atapata nafasi ya kuona aina ya samaki anao wahitaji wanavirutubisho vya aina gani ili kumuongezea uelewa mzuri wa virutubishi vilivyopo katika samaki.
Watalamu hao pia wanateknolojia ya kuzuia wadudu waharibifu katika maharage ambapo kea kutumia majani ya mimea Ambayo haitumii kemikali yeyote na mazao yanakuwa salama kwa miezi mitatu Hadi minne.
"Tunatumia majani ya mimea ya mwarobaini na utupa katika kuhifadhi maharage, majani hayo inatakiwa isagwe vizuri Kisha ikaushwe baadaye mkulima atachanganya na maharage,"alifafanua Joseph Kalonga Mhadhili Msaidizi was ndaki ya sayansi ya kilimo na uvuvi.
0 Comments