Wakulima wa zao la Pamba Kijiji cha Kaseganyama Kata ya
Kasekese Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wameeleza nia yao ya kuachana na
kulima zao hilo kwa msimu wa Kilimo wa Mwaka 2020/2021 kufuatia kuchekeweshewa
malipo yao na mnunuzi wa zao hilo ambapo mpaka sasa hawajalipwa.
Wakiongea kijijini hapo wakulima wa zao la pamba wamebainisha
kuwa licha ya kupima na kupeleka katika ghala la kuhifadhia pamba suala la
malipo yao bado imekuwa kizungumkuti.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando ameongea na
Wakulima wa zao la Pamba katika Kijiji cha Kaseganyama na kueleza kuwa ikifika
siku ya ijumaa hawajalipwa hatua zitachukuliwa dhidi yake
0 Comments