Posts

Showing posts from June, 2026

SUA yahimiza ubunifu kutatua changamoto za jamii

Image
  Na: Ngolo Mboje Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea kusisitiza umuhimu wa ubunifu na matumizi ya maarifa ya vitendo kwa wanafunzi ili kuwawezesha kubuni suluhisho la changamoto mbalimbali za kijamii na kuchangia maendeleo ya taifa.  Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii, SUA, Prof. Agnes Sirima akizungumza na washiriki Akizungumza chuoni hapo Juni 25/2026   kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii, SUA, Prof. Agnes Sirima, amesema chuo kinaendelea kuhimiza wanafunzi kutumia maarifa wanayoyapata darasani na katika mafunzo ya vitendo kuibua bunifu zitakazoongeza thamani ya bidhaa na huduma, kukuza ajira na kuchangia maendeleo ya jamii. Amesema ubunifu unaofanywa na wanafunzi hauwanufaishi wao pekee, bali una mchango mkubwa katika kutatua changamoto za jamii na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi ya nchi. Aidha, amewataka wanafunzi kuendelea kutumia fursa wanazozipata chuo...

Elimu ya SUA yabadilisha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa Wanging’ombe

Image
  Na: Ayoub Mwigune Ufugaji wa ng’ombe wa maziwa katika Kata ya Igima, Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, umeendelea kuwa chanzo muhimu cha mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi, kufuatia kuongezeka kwa uzalishaji na kuboreka kwa ubora wa maziwa kutokana na elimu na tafiti zinazotolewa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Akizungumza kuhusu maendeleo ya ufugaji katika kata hiyo, Afisa Mifugo wa Kata ya Igima, Shazi Moses Okala , amesema kata hiyo ina zaidi ya wafugaji 300 wa ng’ombe wa maziwa, wakiwa na zaidi ya ng’ombe 700. Amesema kwa sasa wafugaji hao huzalisha zaidi ya lita 2,500 za maziwa kwa siku. Amesema maziwa yanayozalishwa hukusanywa kupitia vituo vya ukusanyaji kabla ya kupelekwa kwenye kituo cha kupoozea, na baadaye kusafirishwa kwa ajili ya usindikaji. Okala amesema kabla ya kuanza kwa elimu na utafiti unaotolewa na wataalamu wa SUA kupitia Mradi wa NANOCOM, wafugaji walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali, hususan ugonjwa wa homa ...

Diwani Mstaafu Mbeya apongeza elimu ya SUA katika kupambana na homa ya kiwele

Image
  Na: Ayoub Mwigune    Diwani mstaafu na mfugaji wa ng’ombe wa maziwa, Johnson Kuruwa Mwamdengo kutoka Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, amepongeza juhudi za watafiti na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kuendelea kuwafikia wafugaji mashambani na kuwapatia elimu ya kitaalamu inayolenga kuboresha ufugaji. Akizungumza baada ya kutembelewa na wataalamu hao, Mwamdengo amesema elimu inayotolewa na SUA imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya homa ya kiwele kwa ng’ombe wa maziwa, pamoja na kuboresha uzalishaji na ubora wa maziwa. Amesema mafunzo kuhusu usafi wa mabanda, ukamuaji sahihi na udhibiti wa magonjwa ya mifugo yamewasaidia wafugaji wengi kuimarisha afya ya ng’ombe wao na kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa. Mwamdengo amesema maeneo mengi ya Mkoa wa Mbeya hukumbwa na mvua za muda mrefu, hali inayosababisha mabanda kuwa na unyevunyevu unaoweza kuchochea maambukizi ya homa ya kiwele. Amesema elimu kutoka kwa wataalamu imekuw...

Baraza Kuu la Wafanyakazi SUA lafanya Mkutano Wake wa 136

Image
Na: Asifiwe Mbembela Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) limefanya Mkutano wake wa 136 katika Ukumbi wa Baraza, Kampasi ya Edward Moringe, Morogoro. Katika mkutano huo, wajumbe walipokea na kujadili taarifa mbalimbali   pamoja na masuala yaliyotokana na Mkutano wa 135. Aidha, Baraza Kuu lilipokea na kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chuo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026 pamoja. Hoja na mapendekezo kutoka mabaraza madogo na mikutano ya wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali 17 ya kazi yalisikilizwa na kutolewa ufafanuzi na Menejimenti ya Chuo. Mkutano huo uliangazia pia hoja zilizokamilika ndani ya mwaka husika zikiwemo masuala ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi pamoja na maboresho ya huduma kwa wateja. Aidha, Menejimenti ya SUA ilitoa pongezi kwa wafanyakazi wote kwa ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya Chuo huku likiwatakia kila la heri wajumbe wa kuchaguliwa wa Baraza ...