SUAMEDIA

Vifo vya Mama na Mtoto vitokanavyo na kujifungulia njiani vyaongezeka kwa kukosa huduma ya Afya ya uzazi Kolero-Morogoro

 

Na: Vedasto George

Wananchi wa Kijiji cha Kolero Kata ya Kolero wilayani Morogoro wamesema ubovu wa barabara na kukosekana kwa  Zahanati kijijini hapo kumesababisha kuwepo kwa vifo vingi  vya mama na mtoto vitokanavyo  na kujifungulia njiani wakiwa wanafuata huduma ya Afya ya uzazi katika  Kata   jirani  ya  Duthumi ambayo ipo umbali wa kilometea 25 kutoka kijijini hapo.





Wakizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa aliyefika kwa ajili ya kusiliza chanagoto za wanakijiji hao wamesema   wajawazito hujifungulia njiani na wagonjwa wengine upoteza maisha wakati wanaenda kwenye zahanati hiyo kutokana na umbali pamoja na ubovu wa barabara ambapo nako ukumbana na changamoto ya uchache wa dawa. 



Mganga Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Dtk. Robert Manyerere akatoa maelezo yakina juu ujengwaji wa zahanati katika Kijiji hicho na upatikanaji wa dawa za kutosha katika vituo vya  Afya na Zahanati.


Kutokana na changamoto hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Bakari Msulwa akamtaka Wakala wa Barabara za vijijini na mijini TARURA kuwasilisha mpango kazi unaonyesha lini barabara ya Kolero itatengenezwa na kutoa rai kwa Serikali ya Kijiji na Kata kuwa na tabia ya kuitisha mikutano ili kujadili maendeleo ya Kijiji hicho 



Post a Comment

0 Comments