Posts

Showing posts from August, 2020

Habari Katika Magazeti ya Leo Jumanne September 1

Image
 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo akabidhi Ramani ya Tanzania Inayoonyesha Afya ya Udongo kwa Taha

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya jana (30.08.2020) amefanya kikao na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuendeleza Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacquline  Mkindi jijini Arusha cha kujadili mikakati na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya tasnia ya mboga mboga na matunda (horticulture) nchini. Sambamba na kikao hicho, Katibu Mkuu Kusaya ameikabidhi TAHA zawadi ya Ramani ya Tanzania inayoonesha viwango vya pH na Afya ya Udongo kwa nchi nzima na imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dr. Jacqueline Mkindi. Kusaya ameitaka TAHA kuendelea kuelimisha wakulima wengi zaidi kuzingatia kilimo cha kitaalam kwa kutambua aina ya udongo unaofaa kwa zao husika na mbolea gani itumike, ndio maana amekabidhi ramani hiyo kuwezesha utambuzi wa maeneo yanayofaa kwa mazao ya horticulture nchini. “Tunaendelea kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano mkubwa na wa muda wote inaotupatia wadau wa sekta ya horticulture ” Dr Mkindi alisema. Katibu Mkuu Kusaya alikuwa mkoani A...

Shule ya Mivumoni Islamic yaungua kwa Mara ya 3

Image
  Shule ya Sekondari ya Mivumoni Islamic, iliyopo katika eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni Dar es Salaam, imeteketea kwa moto Alafajiri ya leo Agosti 31, 2020, na kuelezwa kuwa hii ni mara ya tatu shule hiyo kuungua ndani ya kipindi cha miezi miwili. Kamishina Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni Salum Mohamed, amesema kuwa taarifa ya chanzo cha moto huo itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge. "Kwa kipindi cha miezi miwili hili ni tukio la tatu katika shule hii, Julai 18 tulipata tukio la moto la muundo huu na tulizima, Julai 23 tukio la moto tena lilitokea hili ni tukio la tatu mfululizo ndani ya eneo moja, ni matukio ambayo yanaendelea kutokea ndani ya hizi Shule za Kiislamu za Jijini Dar es Salaam, uchunguzi umefanyika na Msemaji wa hili ili kujua chanzo ni nini ataitoa Mkuu wa Mkoa " amesema Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto.

SUA tayari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam kutoa Ushauri na Udahili

Image
  Na: Farida Mkongwe, Dar es Salaam        Wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu wametakiwa kufika katika banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA lililopo kwenye Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam ili waweze kupata ushauri na udahili wa kujiunga na chuo hicho. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Ugani cha Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE kilichopo SUA Dkt. Innocent Babili ambaye ni Mratibu wa Maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia upande wa SUA wakati akizungumza na SUAMEDIA katika maonesho hayo. Dkt. Babil amesema maandalizi yote kwa ujumla yamekamilika na kwamba wananchi watakaofika katika banda hilo la SUA hususan wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu ambao ndio walengwa wakifika watajionea teknolojia mbalimbali zilizopo SUA sanjari na kudahiliwa kwa wale waliokidhi vigezo. “Lengo kubwa hapa ni kuwasaidia vijana waliomaliza kidato cha sita ambao wanata...

Habari Katika Magazeti ya Leo Jumatatu August 31

Image
 

Prof. James Mdoe aridhishwa na maandalizi ya SUA kuwapokea wanafunzi wapya Kampasi ya Mizengopinda Katavi

Image
  Na: Calvin Gwabara,  Katavi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ameridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi na kuanza rasmi kwa Kampasi ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi. Prof. Mdoe ameyasema hayo wakati alipotembelea kampasi hiyo mpya ya SUA iliyopewa jina la Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alipokwenda kujionea maandalizi na mazingira ya kampasi hiyo ambayo inatarajia kupokea wanafunzi tarehe 23/11/2020. Naibu katibu Mkuu huyo amesema uanzishwaji wa Kampasi hiyo unasaidia jitihada za Serikali kupitia Wizara yake kwenye kuongeza nafasi nyingi zaidi za wanafunzi wenye sifa na wanaotaka kusoma elimu ya juu hasa baada ya maboresho makubwa ya elimu yanayofanywa na Serikali nchi nzima kwenye elimu ya Msingi na Sekondari. “ Kwanza niwapongeze sana SUA na uongozi mzima kwa kazi kubwa ambayo mmeshaifanya ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya kampasi hii, ...

SUA, kupitia Kamati ya Kuthibiti Uadilifu ya SUA (KKU-SUA), yaendelea kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake.

Image
  Habari na Mwandishi wetu Ili kuchangia katika utekelezaji wa Awamu ya Tatu (iliyoanza mwaka 2017 na itayomalizika mwaka 2022) ya Mkakati   wa Taifa wa Kupambana na Rushwa, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Kamati ya Kuthibiti Uadilifu ya SUA (KKU-SUA), kimeendelea kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake. Mwenyekiti wa KKU Prof. Mahonge wa pili kulia akiwa na wajumbe wa KKU na wafanyakazi walioshiriki mafunzo katika Kampasi ya Olmotonyi Arusha Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 18 na 19 ya mwezi Agosti mwaka 2020 katika Kampasi za SUA zilizo nje ya Mkoa wa Morogoro, yaani Kampasi ya Olmotonyi mkoani Arusha, na Kampasi ya Mazumbai mkoani Tanga . Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Christopher Mahonge amesema SUA imeazimia kwa dhati kuhakikisha inathibiti uadilifu na kudhibiti rushwa katika maeneo yake ya kazi. Amesema hatua muhimu ya kwanza katika kulifikia lengo hilo, ni kuhakikisha wafanyakazi, hasa waajiriwa wapya, wanaelimishwa kuh...

Teknolojia za Mradi wa RIPAT SUA zawanufaisha wakulima.

Image
   Na: Ayoub Mwigune  Teknolojia mbalimbali zinazotolewa na Mradi unaofahamika kama RIPAT SUA  unaozingatia kuongeza thamani ya mazao na ufugaji unaoshirikisha Shirika la RECODA na Halmashauri ya wilaya ya Mvomero   umewanufaisha wakulima   wengi ndani na nje ya wilaya hiyo        Hayo yamesemwa na wakulima ambao wako kwenye vikundi ambao wamenufaika na mradi wa RIPAT SUA katika wilaya ya Mvomero    wakati walipotembelea na wadau kutoka Wizara ya Kilimo, na wataalamu kutoka SUA      Akiwakabibisha wadau kutoka Wizara ya Kilimo, wataalamu kutoka RECODA, wanafunzi SUA, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii na Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mwakilishi wa kikundi cha Tukaleghoya Bw. Ramadhani Iddi amesema mafanikio makubwa ambayo wameyapata wanakikundi hao ikiwemo ujuzi wa kulima kilimo cha kisasa chenye tija yamewezeshwa na watalaamu hao wa kilimo         Naye mkulima muwezeshaji Bw. Abiasi M...

Kampasi ya Mizengo Pinda - Katavi, kuanza rasmi Muhula mpya wa masomo November 2020

Image
Wakati wanafunzi wakitegemea kuanza rasmi muhula wa masomo katika Kampasi mpya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Kampasi ya Mizengopinda Katavi, chuo kimeendelea kuhakikisha miundombinu yote inakamilika kwa wakati.  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amefanya ziara katika kampasi hiyo ili kuhakikisha miundombinu yote imekamilika kwa wakati na kuwa rafiki kwa wanafunzi wapya watakaoanza masomo yao November 11 2020. Chibunda akiwa kwenye ziara  hiyo amekagua maeneo yote na kujionea maandalizi yakiendelea kwenye Ufungaji wa Vitanda kwenye mabweni, Viti kwenye madarasa, Miundimbinu ya Maji na Umeme kwenye kampasi yote, na marekebisho mengine muhimu ili wanafunzi watakapofika kuwapo chuoni hapo na hivyo kusoma vizuri. Makamu huyo amesema siku ya ijumaa agost 29, 2020 Kampasi hiyo itatembelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Mdoe ambaye atafikia kuona mazingira na namna Chuo hicho kilivyojipanga ku...