SUAMEDIA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare aipongeza SUA kwa Tafiti wanazofanya juu ya Kilimo

 Na. Vedasto George.  
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amekipongeza   Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa tafiti wanazofanya juu ya
kilimo na kusema kuwa chuo hicho kina mchango mkubwa katika 
sekta hii muhimu ya kilimo  na mifugo nchini hasa wakati huu
ambapo taifa limeingia kwenye uchumi wa kati.

Add caption


 Mkuu wa mkoa ameyasema hayo wakati  alipotembelea banda la SUA katika maonesho ya 26 ya wakulima, wafugaji na wavuvi  nanenane ambayo kwa Kanda ya Mashariki yanafanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere mkoani Morogoro. 
“Nimefika hapa kwa sababu ni chuo chetu cha kilimo kwa hiyo
tunatarajia kuona vitu vizuri vinavyotoka SUA, maana tunawafundisha
vijana pia tunawafundisha wakulima wengi sana kuhusu kilimo na
ufugaji”, alisema Sanare. 

“Nafurahi watu wanapita kujifunza maana wataalam hawa wataondoka lakini Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA kipo Morogoro sasa ni kiasi gani sisi tutaendelea kufaidi uwepo wa chuo hiki maeneo yetu, wapo wakulima wengi sana, mkoa wetu wa Morogoro ni mkoa wa kilimo kwa asilimia kubwa tunafaidika na uwepo wa SUA mkoani hapa”, alisistiza mkuu huyo wa mkoa wa Morogoro.
Amesema Agosit 7 mwaka huu akiwa ameambatana  na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo pamoja na  wataalam kutoka wilaya zote za mkoa wa Morogoro atafika rasmi katika maonesho ya wakulima na wafugaji lengo likiwa ni kujionea kazi nzuri inayofanywa na Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA


Maonesho hayo ya 26 ya nanenane yamebeba kauli mbiu isemayo
“Kwa Maendeleo ya Kilimo,  Mifugo na Uvuvi chagua Viongozi Bora
2020”.  

Katika picha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akipata maelezo kuhusiana na kilimo katika Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA alipotembelea katika banda lao ndani ya viwanja vya Mwl.Julius Kambarage Nyerere Nanenane Morogoro jana.

Post a Comment

0 Comments