SUAMEDIA

SUGECO : Vijana waone Kilimo ni Taaluma kama Taaluma nyingine



Na: Farida Mkongwe
Vijana wametakiwa kuelewa kuwa kilimo ni taaluma kama zilivyo
taaluma nyingine na kwamba iwapo watazingatia matumizi ya
teknolojia za kisasa zinazotumika kwenye kilimo basi wanaweza
kupata maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Ushirika wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo  SUGECO Bw. Revocatusi Kimario

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ushirika wa Wahitimu wa
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo  SUGECO Bw. Revocatusi
Kimario wakati akizungumza na SUAMEDIA katika Maonesho ya
Nanenane yanayoendelea kwenye Kanda ya Mashariki mkoani
Morogoro
Bw. Kimario amesema vijana hawana budi kubadilisha fikra
walizonazo kuwa kilimo hakiwezi kumletea mtu maendeleo na
badala yake wanatakiwa kujifunza kupitia vijana wenzao ambao
wameendelea kwa kiasi kikubwa kupitia kilimo.
“Sisi tunachokifanya kwanza ni kubadili fikra walizonazo vijana, wengi hawapendi kilimo lakini kwa sasa tumefanikiwa kubadisha mtazamo wa vijana wengi na sasa wanalima na wanapata faida, wameweza kuwa na maendeleo kwa kiasi kikubwa tu”, alisema Mkurugenzi huyo.
Amesema SUGECO ambayo kwa sasa ina wanachama 960 wengi
wao wakiwa ni wahitimu wa SUA pia inatoa mafunzo ya ujasiriamali
na kuwapeleka vijana nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo ambapo mpaka
sasa wameshawapeleka zaidi ya vijana 225.


Post a Comment

0 Comments