Na: Ayoub Mwigune
Teknolojia mbalimbali zinazotolewa na Mradi unaofahamika kama RIPAT SUA unaozingatia kuongeza thamani ya mazao na ufugaji unaoshirikisha Shirika la RECODA na Halmashauri ya wilaya ya Mvomero umewanufaisha wakulima wengi ndani na nje ya wilaya hiyo
Hayo yamesemwa na wakulima ambao wako kwenye vikundi ambao wamenufaika na mradi wa RIPAT SUA katika wilaya ya Mvomero wakati walipotembelea na wadau kutoka Wizara ya Kilimo, na wataalamu kutoka SUA
Akiwakabibisha wadau kutoka Wizara ya Kilimo, wataalamu kutoka RECODA, wanafunzi SUA, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii na Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mwakilishi wa kikundi cha Tukaleghoya Bw. Ramadhani Iddi amesema mafanikio makubwa ambayo wameyapata wanakikundi hao ikiwemo ujuzi wa kulima kilimo cha kisasa chenye tija yamewezeshwa na watalaamu hao wa kilimo
Naye mkulima muwezeshaji Bw. Abiasi Msinde amesema kuwa katika kuhakikisha teknolojia hiyo inaenea zaidi kikundi chao kinapojifunza kinahakikisha kinawafundisha wakulima ambao sio wanakikundi lengo likiwa ni kuwafikia wakulima wengi na jamii kwa ujumla.
“Binafsi nimewafundisha watu kulima migomba kama wanne na nimewasaidia maotea 40 na wale ambao si wanakikundi wanaendelea kutumia teknolojia kutokana na mafanikio makubwa wanayoipata” amesema Bw. Msinde.
Dkt. Emmanuel Malisa ambaye ni Mratibu wa Mradi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoinecha Kilimo amesema kuna kata saba ambazo mradi tayari umewafikia
0 Comments