Mbegu ya Maharage ya SUA Karanga yatajwa kuongeza tija kwa wakulima
Na: Farida Mkongwe
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari
Mafiga iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kalunde Hamisi,
amesema shule hiyo imeshiriki Maonesho ya Nanenane 2026, kwa kuonesha mbegu
mpya za mazao zilizogunduliwa na watafiti wa SUA.
Kalunde amesema miongoni mwa mbegu hizo ni aina mpya ya maharage inayojulikana kwa jina la SUA Karanga iliyogunduliwa na Prof. Paul Kusolwa, ambayo imezalishwa kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata mazao bora.
Ameeleza kuwa maharage ya SUA Karanga yana sifa mbalimbali,
ikiwemo uwezo wa kuvumilia magonjwa yanayoshambulia zao la maharage pamoja na
kutoa mavuno mengi yakilinganishwa na baadhi ya aina nyingine za maharage.
Kalunde amesema mkulima anayefuata kanuni bora za kilimo anaweza kupata mavuno ya kati ya tani 1.5 hadi tani 3 kwa hekta moja baada ya kupanda mbegu hiyo.
Amewashauri wakulima kutumia mbegu bora ya SUA Karanga ili
kuongeza tija, kipato na faida katika kilimo cha maharage, huku akiwataka
kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu namna sahihi ya kuipanda na kuitunza.
Comments
Post a Comment