Na: Asifiwe Mbembela
Teknolojia hiyo imelenga kuwasaidia wafanyabiashara kuhifadhi mazao yanayoharibika kwa haraka, yakiwemo nyanya, matunda na ndizi, ili kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna na kuyalinda yasiharibike kabla ya kuuzwa.
Wakizungumza
wakati wa kukabidhiwa jokofu hilo, wajasiriamali hao wamesema awali walikuwa
wakipata hasara kutokana na mazao kuiva na kuoza ndani ya siku chache endapo
hayakuuzwa kwa wakati.
Mmoja
wa wanufaika wa teknolojia hiyo, Bi. Zainabu Ally mwenye umri wa miaka 31,
anayefanya biashara ya nyanya, amesema kuharibika kwa mazao kulikuwa
kukisababisha kupoteza sehemu ya mtaji na wakati mwingine kulazimika kusitisha
biashara.
“Tulikuwa tunapata wakati mgumu kwa sababu usipouza kwa wakati, nyanya zako zinaanza kuoza na unalazimika kuziuza hata kwa hasara,” amesema Zainabu.
Kiongozi
wa Mradi huo, Dkt. Nuria Majaliwa, amesema teknolojia hiyo ina uwezo wa
kuhifadhi nyanya na matunda kwa kipindi cha hadi wiki mbili, sawa na siku 14,
hivyo kusaidia kupunguza upotevu wa mazao na hasara kwa wafanyabiashara.
Teknolojia
hiyo inatarajiwa kuchangia katika kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna,
kulinda mitaji na kuongeza kipato cha wajasiriamali wadogo katika Soko la
Lukole na maeneo mengine yatakayofikiwa.

.jpg)

.jpg)


0 Comments