Na: Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni
na Michezo, Bi. Husna Juma, amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) kwa kuendelea kutumia utaalamu, tafiti na ubunifu katika kutatua
changamoto za jamii na kuchochea maendeleo ya Taifa.
Bi. Husna ametoa pongezi hizo Agosti 19, 2026, alipotembelea Banda la SUA katika Maonesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea jijini Tanga, ambapo alipata fursa ya kujionea tafiti, bunifu na teknolojia mbalimbali zinazowasilishwa na Chuo hicho.
Mwenyekiti huyo alitoa pongezi
za dhati kwa wataalamu na Jumuiya nzima ya SUA kwa kuendelea kuonesha ubunifu,
weledi na kujitoa katika kuendeleza elimu, utafiti na uvumbuzi. Alisisitiza
umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika maarifa na bunifu zenye tija kwa jamii na
Taifa.
Aidha, Bi. Husna aliipongeza Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika SUA, akieleza kuwa uwekezaji huo umewezesha Chuo kuimarisha miundombinu, tafiti, ubunifu na uwezo wa wataalamu, hatua inayochangia SUA kutoa suluhisho za kisayansi na kiteknolojia kwa changamoto mbalimbali za maendeleo nchini.






0 Comments