AGCOT yaipongeza SUA kwa mchango katika Kilimo biashara
Na: Ngolo Mboje
Taasisi
ya Kilimo ya AGCOT imepongeza mchango mkubwa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) katika kuendeleza kilimo biashara kupitia ushirikiano wa mafunzo,
utafiti na kuwajengea uwezo wakulima pamoja na wajasiriamali nchini.
Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane, mwakilishi wa AGCOT, Bw. Adam Ndatulu, amesema taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali, wakiwemo SUA na IUCN, ili kuhakikisha wakulima na wajasiriamali wanapata mafunzo yanayowawezesha kuongeza tija na thamani ya mazao yao.
Amesema
mafunzo hayo yamechangia kuwasaidia washiriki kuanzisha na kuendesha shughuli
mbalimbali za kilimobiashara, ikiwemo viwanda vya kukamua mafuta na uzalishaji
wa asali, hatua inayochochea ukuaji wa uchumi katika jamii.
Bw. Ndatulu ameishukuru SUA kwa ushirikiano wake wa muda mrefu, akieleza kuwa chuo hicho kimekuwa kikipeleka wanafunzi kufanya mafunzo kwa vitendo katika taasisi hiyo, jambo linalowajengea vijana ujuzi, uzoefu wa kazi na kuwafanya kuwa sehemu ya maendeleo ya sekta ya kilimobiashara.
Aidha,
amesema ushirikiano kati ya taasisi hizo umewezesha utekelezaji wa ajenda
mbalimbali za mazingira na maendeleo ya kilimo, huku wataalamu wa SUA
wakiendelea kutoa ushauri na mawazo ya kitaalamu yanayosaidia kuboresha
shughuli za kila siku za AGCOT.
“SUA
imekuwa mdau muhimu katika shughuli zetu, mawazo yao yamekuwa chanya na
yametusaidia kuendesha ajenda mbalimbali za mazingira na maendeleo ya kilimo
kwa ufanisi,” amesema Bw. Ndatulu.
Comments
Post a Comment