Habari za leo ndugu msomaji wangu na pole kwa shughuri mbalimbali za ujenzi wa Taifa. Unapoanzisha mradi unatarajia mwisho wa siku uumalize kwa kupata faida, sasa basi leo nataka nikufahamishe mambo makubwa mawili unayotakiwa kuyajua kabla hujaanza mradi wako wowote wa kilimo.
Jambo la kwanza: Farming master-plan
Hili ni jambo la kwanza na muhimu sana kulifahamu. Farming master-plan ni muongozo wa shughuri zote unazotakiwa kuzifanya katika kilimo chako tangu kuandaa shamba mpaka kuvuna. Hii ijumuishe shughuri kama kupanda, kudhibiti magugu, uwekaji wa mbolea na kupulizia madawa ya wadudu na magonjwa. Unatakiwa kujua shughuri hizi zote, muda wa kuzifanya, namna ya kuzifanya na mahitaji yake ili uzifanye.
Kwa mfano uwekaji wa mbolea: wakati gani uweke? kiasi gani? uwekeje? Unatakiwa ufahamu haya yote kabla hujaanza mradi wako wa kilimo ili usipate usumbufu wakati wa utekelezaji.
Jambo la pili: Gharama za uzalishaji na makadirio ya faida
Hili ni jambo lingine muhimu sana. Najua hujaamua kulima ili ujifurahishe tu, unatafuta faida hivyo basi unatakiwa ujue mradi wako utakugharimu kiasi gani katika utekelezaji wake na mwisho wa siku utakulipa kiasi gani? Pengine hutopata gharama halisi lakini ni lazima ufahamu japo makadirio ya gharama ili kwanza uweze kujipanga lakini pia usikwame katika utekelezaji wa mradi wako.
Kwanini ni muhimu kufahamu mambo haya?
Utajua mahitaji muhimu unayotakiwa kuwa nayo kabla hujauanza mradi wa kilimo
Utapata fursa ya kuuona mradi wako katika hatua mbalimbali hata kabla hujauanzisha
Utaweza kujua makadirio ya gharama za uzalishaji na faida tarajiwa. Kwa hiyo nikusihi ndugu yangu usianzishe mradi wako wa kilimo mpaka ujiridhishe kuwa unayafahmu mambo haya mawili.

0 Comments