Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelipongeza shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa kuanzisaha mfumo wa mawasiliano utakaowasaidia wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo nchini.
Rais Magufuli ameota pongezi hizo May 21 wakati wa hafla ya kupokea gawio la Serikali kwa mujibu wa sheria kutoka shirika hilo ambapo limetoa jumla ya shilingi bilioni2.1
Aidha Rais Magufuli ameonesha kushangazwa na Shirika hilo kuendelea kukodisha minara ya mwasiliano katika Mikoa mbalimbali wakati linatakiwa kuwa na minara yake na kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Injiania Isack kamwelwe kuhakikisha wanapata fedha ili kujengwa minara watakayopewa TTCL.
0 Comments