SUAMEDIA

LUGOLA-Ni marufuku kwa Taasisi yeyote nchini kuandaa maandamano

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola, amesema ni marufuku kwa Taasisi yeyote nchini kuandaa maandamano yanayoweza kuleta machafuko na kuvuruga amani.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, leo. 
 Akizungumza na Waandishi wa habari May 19 katika ukumbi wa mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, Mjini Morogoro, Waziri Lugola ametoa msimamo huo kufuatia kuwepo kwa tetesi za madereva wa mabasi yaendayo mikoani kutaka kufanya mgomo

Lugola amesema kumekuwa na madai ya madereva hao kutokuwa na mikataba ya ajira, kukamatwa ovyo na askari wa kikosi cha Usalama barabarani na tozo mbalimbali wanazoona sio haki kuzilipa

Waziri huyo wa Mambo ya Ndani amesema kero hizo zinashughulikiwa

Amesema Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ni sikivu, na baada ya kupata malalamiko  viongozi hao wamekutana ili kupata suluhisho ya malalamiko yao.

Lugola amesema kabla ya kuzungumza na waandishi hao, walifanya kikao Mei 18, 2019 na wadau wa usafirishaji nchini, ambao ni Chama cha Wamiliki wa Mabasi, Wamiliki wa Malori, Chama cha Madereva na wadau wengine



Waziri Lugola ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh. Antony Mavunde, Wawakilishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), na Jeshi la Polisi, walikubaliana na viongozi wenzake kukutana tena kwa ajili ya kupata suluhisho ya baadhi ya malalamiko ya wadau hao ikiwemo lalamiko la kudhibiti mwendo.

“Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ni sikivu ndiyo mana tumekutana hapa, tunawaagiza wamiliki wa vyombo vya moto nchini kutoa mikataba ya kazi kwa madereva na wafanyakazi mbalimbali katika makampuni yao, tochi zipigwe kjwa weledi na si kuwaonea madreva kwakutoonekana picha ya gari lililofanya kosa, kusimishwa hovyo barabarani pamoja na kutosimamisha mabasi ambayo yana abiria.


Lugola ameongeza kuwa, mgomo wa aina yoyote ni ukiukwaji wa Sheria za nchi hivyo ni marufuku kufanya jaribio hilo ambalo lilitishiwa kufanywa.

Post a Comment

0 Comments