Prof . Amandus Mhairwa Mkuu wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine amewataka watanzania wanaojihusisha na ufugaji wa kuku kushirikiana kwa pamoja kutokomeza magonjwa ya kuku ikiwemo mdonde .
Ameyasema hayo akiwa katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika chuo hicho cha SUA katika uchunguzi wa magonjwa ya kuku hasa katika upande wa mdonde kwani ugonjwa huwo ndio ugonjwa mkubwa unaowasumbua kuku katika jamii mbalimbali
Ameongezea kwa kusema kuwa yapo magonjwa mengine mengi yanayowasumbua wafugaji wa kuku katika maeneo mbalimbali hapa nchini hivyo wafugaji wanatakiwa kuwa makini katika ufugaji
ametoa ushauri kwa wafugaji wa kuku na amesema kuwa hakuna madhara makubwa ambayo yanampata mtu anapokula nyama ya kuku mwenye ugonjwa wa mdonde na magonjw mengine
0 Comments