SUAMEDIA

FAHAMU NJIA BORA ZA UFUGAJI WA MBUZI

Ili uweze kuwa mfugaji bora wa mbuzi yapo mambo ya muhimu unayopaswa kuyafahamu, mambo hayo yatakusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kusonga mbele kwenye suala la mafanikio ya kiufugaji.

Yafutayo ndiyo mambo ya msingi ya kuzingatia katika ufuagaji wa mbuzi.

Namna bora ya ufugaji.
1. Wafugwe kwenye banda bora.
2. Chagua  mbuzi kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji (uzalishaji) nyama au maziwa.
3. Walishwe chakula sahihi kulingana na umri wa mbuzi.
4. Kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa hili ni jambo la muhimu sana.
5. Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.
6. Kuzalisha nyama au maziwa bora yanaokidhi mahitaji ya soko.

Sifa za banda bora la kufugia mbuzi.
1. Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali (hatari) na wezi.
2. Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.
3. Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.
4. Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.

Kama utafuga mbuzi kwa kuwafungia (shadidi) muda wote zingatia yafuatayo:-
1. Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua.
2. Lenye hewa ya kutosha.
3. Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya kuwekea chakula na maji.
4. Liwe na vyumba tofauti kwa kuweka vijitoto/wanao ugua/wanao kua.

Ujenzi wa banda la mbuzi.
1. Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo husika na kwa kuzingatia uwezo wa mfugaji.
2. Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwanga na hewa ya kutosha.
3. Mlango uwe na ukubwa wa 60X150 sentimeta.
4. Sakafu iwe ya udongo/zege ya kichanja unaweza kutumia mabanzi/mianzi na iruhusu kinyesi na mikojo kudondoka chini.
5. Chumba cha majike na vitoto kiwe na sentimeta 1.25kati ya fito na fito au papi na papi, chumba cha mbuzi wakubwa kiwe na sentimeta 1.9 kati ya mbao na mbao.

KWAHISANI YA MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments