Na: Calvin Gwabara – Nairobi.
Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa
Teknolojia za Kilimo Barani Afrika wamezimia mkutano wa pili wa ACAT ufanyike
Jijini Kigali ncnhini Rwanada.
Hilo limesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Teknolojia za Kilimo
Afrika (AATF) Dkt. Canisius Kanangire wakati akisoma maazimio ya mkutano huo
kwa niaba ya washiriki wote zaidi ya 500 kutoka nchi mbalimbali za afrika na nje
ya Afrika.
“Kwa pamoja wadau wa mkutano huu ambao
utakuwa unafanyika kila baada ya miaka miwili tumekubaliana kukutana tena kukutana tena mjini Kigali, Rwanda kuanzia tarehe 19 - 23
Mei, 2025 ili kutathmini yale ambayo tumekubaliana kuyafanya kila mmoja wetu na
wadau” Alieleza Dkt. Kanangire.
Aidha
amesema wadau wamepitisha ACAT kuwa kongamano la kila baada ya miaka miwili
katika bara litakaloonyesha teknolojia na ubunifu zinazoibukia, uanzishaji wa
mitandao na kufungua ufikiaji wa teknolojia na uhauwilishaji wake.
Wametoa
wito kwa Umoja wa Afrika (AU) kutambua na kushirikisha taasisi ambazo zimefanya
vyema katika nyanja ya maendeleo na usambazaji wa Teknolojia za Kilimo kama
vile AATF kama mshauri wao wa kiufundi katika masuala ya Teknolojia ya Kilimo.
Pia maazimio hayo yametaka kurejelea hitaji la uwekezaji katika shughuli zinazounga
mkono ufanyaji biashara na upitishaji wa teknolojia za kilimo ikiwa ni pamoja
na kuimarisha huduma za ugani, kuzalisha bidhaa zenye ufanisi na kuondoa vikwazo
vya Kitarifuna zisizo za tarifu.
Pia
wametoa wito wa kupunguzwa athari hasi za ongezeko mashirika yasiyo ya
kiserikali (NGOs) zinazopinga uvumbuzi wa kiteknolojia wa riwaya ikijumuisha
viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMOs) barani Afrika kupitia majadiliano
yenye kujenga na ushirikishwaji wa malengo, unaoungwa mkono na ushahidi wa
kisayansi badala ya upotoshwaji usio na ushahidi.
PICHA ZA WADAU WAKIFUATILIA MAAZIMIO YA MKUTANO HUO.
0 Comments