SUAMEDIA

SUA imendelea kuwapa motisha wanafunzi , wafanyakazi ili kufikia malengo yao


Na, Editha Mloli

 Ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo na wafanyakazi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) umekuwa na motisha kwa  kuendelea kufanya vizuri na kukipa sifa nzuri ndani na nje ya Chuo hicho hivyo kukifanya chuo kuwa chachu kwa Vyuo vingine hapa nchini.



 Sanjari na hayo ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi hao uliambatana na ugawaji wa zawadi kwa Watafiti wanaofanya vizuri kutoka SUA ambao wamekuwa na nafasi kubwa ya kukiletea heshima Chuo hicho lakini pia kukiongezea kipato ambapo haya yamedhihirika  Novemba 21, 2023 katika zoezi la ugawaji zawadi kwa watafiti hao pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao.

 Hayo yamezungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Rafael Chibunda wakati akizungumza katika ukumbi wa Multipurpose uliopo Chuoni hapo wakati akimkaribisha Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Caroline Nombo.

 Prof. Chibunda amesema wanajivunia wanafunzi wao kufanya vizuri kila mwaka na hii inadhihirisha wazi kuwa Chuo hicho kimeaandaa wanafunzi Bora na waliobobea kinadharia na vitendo wanaoweza kujiajiri bila kutegemea kuajiriwa.

 Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Carolyne Nombo amewataka wanafunzi wanaopokea zawadi hizo watumie Elimu zao na kubadilisha taaluma walioipata katika kusaidia jamii kutatua changamoto wanazokumbana nazo katika kuleta maendeleo.

 Zoezi hili la ugawaji zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri SUA lilianza mwaka 1998 na limekuwa endelevu kila mwaka na utamaduni huu utaendelea kuwa chachu hata kwa wanafunzi wanaosoma chuoni hapo na hata wale ambao wanatamani kuja kusoma SUA hapo baadae.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Elimu Prof. Nombo ameahidi kuchangia utoaji wa zawadi kwa Mtafiti Bora wa kike kutoka SUA.




 















KATIKA VIDEO

Post a Comment

0 Comments