Posts

SUA Media yatwaa tuzo kwa ushiriki katika Kongamano la Kiswahili Duniani

Image
  Na: Farida Mkongwe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia SUA Media kimeendelea kujipambanua katika tasnia ya habari baada ya kutunukiwa tuzo maalum ya ushiriki katika Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili Duniani lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) . Tuzo hiyo iliyotolewa jijini Arusha Machi 26, 2026 inaakisi utambuzi wa mchango mkubwa wa vyombo vya habari, ikiwemo SUA Media, katika kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha matumizi sahihi ya lugha adhimu ya Kiswahili Akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) , Mhadhiri Mwandamizi Dkt. Onesmo Nyinondi , ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Taaluma za Lugha, ameipongeza SUA Media kwa mafanikio hayo. Amesema kuwa ushiriki wa chuo katika majukwaa ya kimataifa kama hayo unaongeza mwonekano wa SUA na kuonesha kuwa chuo hakijajikita tu katika kilimo na sayansi ngumu, bali pia kina mchango mkubwa katika sayansi ya lugha na mawasiliano. “SUA tukiendelea kushiriki kwenye maj...

Serikali yaimarisha Kiswahili kimataifa kupitia teknolojia na fursa za ajira

Image
  Na: Farida Mkongwe Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kukuza na kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili kupitia fursa mbalimbali zikiwemo ukalimani, tafsiri, uhariri, uandishi, utangazaji wa habari na ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni kwa lengo la kuiwezesha lugha ya Kiswahili kuwa chombo muhimu cha ajira na uchumi kwa watanzania. Akizungumza jijini Arusha Machi 24, 2026, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Mhe. Makonda amesema Serikali imefanikiwa kupanua wigo wa ufundishaji wa Kiswahili kwa kufungua vituo 20 nje ya nchi kupitia balozi za Tanzania na vituo 35 ndani ya nchi, idadi ambayo imeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka vituo viwili vya nje ya nchi na vitatu vya ndani vilivyokuwepo miaka mitano iliyopita. Aidha, Waziri Makonda amesema Tanzania inaendelea kuwa kinara katika kukuza Kis...

Mradi wa CERA waimarisha utafiti wa Mpunga kwa kuwajengea uwezo wakusanyaji takwimu.

Image
  Na: Calvin Gwabara – Morogoro Tanzania. Mradi wa Mpunga Himilivu kwa mabadiliko ya Tabianchi na Rafiki kwa Mazingira Barani Afrika (Climate-resilient and Eco-friendly Rice for Africa) (CERA) umechukua hatua muhimu katika kuboresha kilimo cha mpunga kwa kuendesha mafunzo maalum kwa wakusanyaji takwimu katika utafiti unaotarajia kufanyika kwenye Mikoa ya Morogoro, Shinyanga na Songwe nchini Tanzania. Mtafiti Mkuu wa mradi Prof. Suzana Nchimbi Msolla akizungumza na watafiti hao kabla ya kuanza zoezi hilo. Mafunzo hayo yamewaleta pamoja washiriki ambao watakuwa mstari wa mbele katika ukusanyaji wa taarifa kutoka kwa wakulima, hatua inayotarajiwa kusaidia kufanya maamuzi sahihi ya kisayansi kwenye utekelezaji wa mradi huo wa utafiti. Akizungumza na watafiti hao wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mtafiti Mkuu wa mradi Prof. Suzana Nchimbi Msolla alitumia nafasi hiyo kueleza kwa kina kuhusu mradi wa CERA, akieleza malengo, muda wake pamoja na matarajio yake hasa katika  kuim...

Waziri Mkuu aweka jiwe la msingi jengo la taaluma na bweni SUA

Image
  Na: Mwandishi wetu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kinaendelea kuimarisha miundombinu ya elimu katika Kampasi ya Mizengo Pinda kupitia ujenzi wa jengo la taaluma na bweni la wanafunzi kwa ufadhili wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi iliyofanyika tarehe 14 Machi, 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu ya juu ili kuongeza ubora wa mafunzo, tafiti na huduma kwa jamii. Aidha, Waziri Mkuu amewahimiza wanafunzi kutumia kikamilifu fursa ya maboresho ya miundombinu ya elimu yanayofanywa na Serikali kwa kusoma kwa bidii na kujenga msingi imara wa taaluma zao ili waweze kuchangia maendeleo ya taifa. Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Prof. Maulid Mwatawala, akimwakilish...

Waziri Mkuu kuweka jiwe la msingi la majengo ya taaluma na bweni SUA – Kampasi ya Mizengo Pinda

Image
  Na: Asifiwe Mbembela Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kikili (SUA) kinatarajia kuandika historia mpya kufuatia kufanyika kwa Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Bweni katika Kampasi ya Mizengo Pinda, itakayofanyika siku ya Jumamosi, tarehe 14 Machi, 2026. Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye anatarajiwa kuweka jiwe la msingi kuashiria mwanzo wa utekelezaji wa mradi huo muhimu wa kimkakati. Ujenzi wa majengo hayo unatekelezwa kwa ufadhili wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaolenga kuimarisha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia vyuo vikuu nchini. Mradi huu pia utaboresha mazingira ya malazi kwa wanafunzi na hivyo kuongeza ufanisi wa shughuli za kitaaluma pamoja na ustawi wa wanachuo kwa ujumla. Kupitia mradi huu, Chuo kitaongeza uwezo wa kuhudumia wanafunzi wengi zaidi sambamba na kuboresha ubora wa mazingira ya kujifunzia, jambo litakalochochea maen...

Wanawake wa SUA waonesha upendo kwa jamii ya Kauzeni kupitia matendo ya huruma

Image
  Na: Farida Mkongwe Wanawake wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na wafanyakazi wengine wa chuo hicho wamefanya matendo ya huruma kwa kutoa misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo nguo, sukari, unga, sabuni na mafuta kwa wahitaji wa Kata ya Kauzeni iliyopo Manispaa ya Morogoro pamoja na Kituo cha Watoto cha Sarafina kilichopo katika kata hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, kwa lengo la kuonesha upendo na mshikamano kwa jamii. Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU Tawi la SUA ambaye pia ni mratibu wa shughuli hiyo, Bi. Enessa Mlay, amesema wanawake wa SUA wameona umuhimu wa kuadhimisha siku hiyo kwa vitendo kwa kuwafikia wananchi wanaohitaji msaada ili kuonesha mshikamano kwa jamii kwa kufanya matendo ya huruma. “Kipindi hiki ni cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresima, ambacho tunahimizwa kufanya matendo mema na kusaidiana katika jamii, lengo let...

TPHPA kuimarisha huduma Njombe kwa kujenga maabara ya kisasa.

Image
 Na: Mwandishi wetu - Njombe. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya, Mimea na Viwatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru. Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka (wa kwanza kulia) akiwa na timu ya wataalamu kutoka TPHPA ikiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu Prof. Joseph Ndunguru (wa kwaza kushoto). Lengo kuu la mazungumzo hayo likiwa kumkabidhi mkandarasi kwa ajili ya usanifu wa michoro na usimamizi wa ujenzi wa Maabara ya Kimkakati pamoja na jengo la utawala, ambayo yatajengwa katika Mji wa Serikali Lunyanywi. Katika mazungumzo hayo, Prof. Ndunguru alieleza kuwa TPHPA imesaini mkataba wa kupeleka bidhaa 60 nchini Malawi, zikiwemo aina 30 za mazao yatakayosafirishwa huko. Mhe. Mtaka alimshukuru Prof. Ndunguru kwa kutambua kuwa Njombe ni miongoni mwa mikoa inayozalisha chakula kwa wingi, hivyo kuna umuhimu wa kujenga maabara ya kimkakati itakayosaidia wakulima na wafanyabiashara kupata huduma bo...