Na: Mwandishi wetu - Njombe.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amekutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya, Mimea na Viwatilifu Tanzania (TPHPA), Prof.
Joseph Ndunguru.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka (wa kwanza kulia) akiwa na timu ya wataalamu kutoka TPHPA ikiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu Prof. Joseph Ndunguru (wa kwaza kushoto). |
Katika
mazungumzo hayo, Prof. Ndunguru alieleza kuwa TPHPA imesaini mkataba wa
kupeleka bidhaa 60 nchini Malawi, zikiwemo aina 30 za mazao yatakayosafirishwa
huko.
Mhe.
Mtaka alimshukuru Prof. Ndunguru kwa kutambua kuwa Njombe ni miongoni mwa mikoa
inayozalisha chakula kwa wingi, hivyo kuna umuhimu wa kujenga maabara ya
kimkakati itakayosaidia wakulima na wafanyabiashara kupata huduma bora za
kisayansi na kiuchumi.
MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA KIKAO HICHO.

.jpeg)



0 Comments