Mradi wa Utafiti wa "FETE" kuja na majibu ya Mazingira ya Chakula na Lishe kwa nchi zinazoendelea.
Na: Calvin Gwabara – Morogoro. Jopo la Watafiti katika Mradi wa Utafiti wa Mazingira ya Chakula katika Miji na kuboresha lishe ya Walaji (FETE) wamekutana kuzindua mradi na kupanga mikakati ambayo itasaidia kuimarisha lishe ya jamii na kupunguza utapiamlo kwa nchi nne za Afrika zinazoshiriki utafiti huo. Mtafiti Mkuu wa mradi wa utafiti wa (FETE) kwa upande wa Tanzania Prof. Joyce Kinabo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo. Hayo yamebainishwa na Mtafiti Mkuu wa mradi huo kwa upande wa Tanzania Prof. Joyce Kinabo ambaye ni Profesa wa lishe wakati akitoa utambulisho wa Mradi huo kwa jopo hilo linalohusisha watafiti kutoka Tanzania, Ghana, Afrika ya Kusini,Malaysia na Ujerumani kwa ufadhili wa Shirikisho la Shirika la Kilimo na Chakula la Ujerumani (BLE). “Wengi mtakubaliana na mimi kuwa tuna matatizo makubwa ya utapiamlo wa chini na utapiamlo wa juu kwa maana kwamba uzito ulikithiri na unene unazidi kuwa changamoto kwa watu wengi hapa Tanzania changamoto ambayo inachang...