SUA yabuni mfumo wa AI wa kuhesabu vifaranga vya samaki
Na: Ngolo Mboje Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimebuni teknolojia ya akili unde (AI) ijulikanayo kama Tilapia Fingerling Counter, inayowezesha kuhesabu vifaranga vya samaki kwa kutumia simu ya mkononi kwa haraka na kwa usahihi. Ubunifu huo unalenga kurahisisha zoezi la kuhesabu vifaranga na kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa shughuli hiyo. Akizungumza na SUA Media wakati wa Maonesho ya Nanenane, Mhadhiri Msaidizi kutoka Idara ya Uzalishaji wa Viumbe wa Majini na Malisho, Magoti Ernest, amesema mfumo huo unawasaidia wafugaji wa samaki kuhesabu vifaranga kwa muda mfupi na kuongeza uhakika wa idadi wakati wa kufanya biashara. Ernest ameeleza kuwa mfumo huo huchukua takribani dakika tano kukamilisha zoezi la kuhesabu vifaranga, hivyo kuokoa muda unaoweza kutumika katika shughuli nyingine za uzalishaji. “Teknolojia hii inapunguza muda wa kazi, inaongeza usahihi wa hesabu na kumwezesha mfugaji kuendelea na shughuli nyingine kwa haraka,” amesema. Aidha, ames...
Comments
Post a Comment