Na.Vedasto George.
DUNIA inatarajiwa kuwa na upungufu mkubwa wa chakula ifikapo mwaka 2030 kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, ambapo hali hiyo itasababisha watu zaidi million 800 kukumbwa na baa la njaa, hivyo jitihada za ziada kwenye utafiti wa kilimo zinahitajika ili kukabiliana na hali hiyo.
Hayo yamebainishwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA Prof. Maulid Mwatawala kulingana na ripoti ya shirika la chakula duniani ya mwaka 2020 Mjini Morogoro wakati akifungua kongamano la wadau wa kilimo ambalo linajadili masuala mbalimbali ya kuboresha kilimo ikolojia.
0 Comments