SUAMEDIA

Baraza Kuu la Wafanyakazi SUA lafanya Mkutano Wake wa 136

Na: Asifiwe Mbembela

Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) limefanya Mkutano wake wa 136 katika Ukumbi wa Baraza, Kampasi ya Edward Moringe, Morogoro.

Katika mkutano huo, wajumbe walipokea na kujadili taarifa mbalimbali  pamoja na masuala yaliyotokana na Mkutano wa 135.

Aidha, Baraza Kuu lilipokea na kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chuo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026 pamoja.

Hoja na mapendekezo kutoka mabaraza madogo na mikutano ya wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali 17 ya kazi yalisikilizwa na kutolewa ufafanuzi na Menejimenti ya Chuo.

Mkutano huo uliangazia pia hoja zilizokamilika ndani ya mwaka husika zikiwemo masuala ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi pamoja na maboresho ya huduma kwa wateja.

Aidha, Menejimenti ya SUA ilitoa pongezi kwa wafanyakazi wote kwa ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya Chuo huku likiwatakia kila la heri wajumbe wa kuchaguliwa wa Baraza la 136 ambao wamemaliza muda wao.

Kabla ya Mkutano huo wajumbe walifanya ziara ya kutembelea Miradi ya Chuo iliyopo Kampasi ya Solomon Mahlangu iliyopo Mazimbu na Kampasi Kuu ya Edward Moringe. 







Post a Comment

0 Comments