Na: Ayoub Mwigune
Akizungumza baada ya kutembelewa na wataalamu hao, Mwamdengo amesema elimu inayotolewa na SUA imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya homa ya kiwele kwa ng’ombe wa maziwa, pamoja na kuboresha uzalishaji na ubora wa maziwa.
Amesema
mafunzo kuhusu usafi wa mabanda, ukamuaji sahihi na udhibiti wa magonjwa ya
mifugo yamewasaidia wafugaji wengi kuimarisha afya ya ng’ombe wao na kuongeza tija
katika uzalishaji wa maziwa.
Mwamdengo
amesema maeneo mengi ya Mkoa wa Mbeya hukumbwa na mvua za muda mrefu, hali
inayosababisha mabanda kuwa na unyevunyevu unaoweza kuchochea maambukizi ya
homa ya kiwele. Amesema elimu kutoka kwa wataalamu imekuwa na mchango mkubwa
katika kuwawezesha wafugaji kukabiliana na changamoto hiyo.
“Tunazipongeza tafiti hizi zinazoendelea, na tunaamini zitatoa suluhisho zaidi kwa changamoto hii ili kuwasaidia wafugaji kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa yanayopelekwa sokoni,” amesema Mwamdengo.
Aidha,
amesema mafunzo kuhusu lishe bora ya mifugo yamewasaidia wafugaji kutumia
vizuri rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao, ikiwemo majani, mabua ya
migomba na virutubisho vingine, jambo lililochangia kuimarisha afya ya mifugo
na kuongeza uzalishaji wa maziwa.
Mwamdengo amesema kuendelea kwa
ushirikiano kati ya watafiti wa SUA na wafugaji kutasaidia kutatua changamoto
mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya mifugo, na hivyo kuongeza mchango wa
sekta hiyo katika uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.




0 Comments