Na: Ngolo Mboje
Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea kusisitiza umuhimu wa ubunifu na
matumizi ya maarifa ya vitendo kwa wanafunzi ili kuwawezesha kubuni suluhisho la
changamoto mbalimbali za kijamii na kuchangia maendeleo ya taifa.
![]() |
| Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii, SUA, Prof. Agnes Sirima akizungumza na washiriki |
Akizungumza chuoni hapo Juni 25/2026 kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii, SUA, Prof. Agnes Sirima, amesema chuo kinaendelea kuhimiza wanafunzi kutumia maarifa wanayoyapata darasani na katika mafunzo ya vitendo kuibua bunifu zitakazoongeza thamani ya bidhaa na huduma, kukuza ajira na kuchangia maendeleo ya jamii.
Amesema
ubunifu unaofanywa na wanafunzi hauwanufaishi wao pekee, bali una mchango
mkubwa katika kutatua changamoto za jamii na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi
ya nchi. Aidha, amewataka wanafunzi kuendelea kutumia fursa wanazozipata chuoni
kukuza uwezo wao wa ubunifu na ujasiriamali.
![]() |
| Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii, SUA, Prof. Agnes Sirima akisikiliza maelezo kutoka kwa Magoti Ernest, mmoja wa wanufaika wa SUA Innovation Hub |
Kwa
upande wake, Mratibu wa Kituo cha Ubunifu ‘SUA Inovation Hub’ SUA, Dkt. Doreen
Ndossi, amesema kituo hicho kinaendelea kuwa jukwaa la kulea na kuendeleza
wabunifu kwa kuwapatia mafunzo, ushauri wa kitaalamu na kuwaunganisha na fursa
mbalimbali zitakazowawezesha kukuza bunifu zao.
Dkt.
Ndossi amewapongeza wabunifu walioshiriki katika maonesho hayo kwa kuonesha
uwezo mkubwa wa kutumia ubunifu na teknolojia kutatua changamoto mbalimbali,
huku akiwahimiza wanafunzi na vijana wengine kujitokeza kushirikiana na Sua Innovation Hub ili kupata mwongozo na msaada
wa kitaalamu utakaowawezesha kubadilisha mawazo yao kuwa bidhaa na huduma zenye
manufaa kwa jamii.
![]() |
| Mratibu wa Kituo cha Ubunifu ‘SUA Inovation Hub’ SUA, Dkt. Doreen Ndossi akitoa maelezo juu ya Inovation Hub |
Kwa
upande wake,Ndg. Magoti Ernest, mmoja wa wanufaika wa SUA Innovation Hub na
mlezi wa wabunifu, amesema mafanikio aliyoyapata yametokana na malezi na
ushauri alioupata alipokuwa mwanafunzi chuoni hapo.
Magoti
amewataka watumishi wa chuo kuendelea kuwaunga mkono wanafunzi wenye mawazo
bunifu ili yaweze kugeuka kuwa teknolojia na biashara zinazoweza kutatua
changamoto za jamii.
Amesema
mafanikio hayo yanaonesha uwezo mkubwa wa wanafunzi wa Sua katika ubunifu na kwamba, kwa kuendelea kupata
ushauri na mazingira rafiki ya kujifunza, wanaweza kufanya vizuri zaidi katika
ngazi ya kitaifa na kimataifa.




0 Comments