NA: Nichorous Romani
Mashindano ya Michezo kwa Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) maarufu kama Chibunda CUP Msimu wa Sita yamefunguliwa rasmi leo tarehe 23/09/2022 katika Viwanja vya Michezo vya Kampasi ya Edward Moringe Sokoine mkoani Morogoro.
Akifungua mashindano hayo Prof. Samweli Kabote
akimuwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof: Raphael Chibunda
amesema kuwa mashindano hayo yanasaidia
kuwakutanisha pamoja watumishi wa Chuo hicho
ikiambatana na kuimarisha afya zao ambapo itawasaidia kufanya kazi kwa
ufanisi bila kusumbuliwa na magonjwa yanayosababishwa na mtindo wa maisha.
Pamoja na hayo Prof. Kabote ameongeza
kuwa mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka na yamendelea kuwa na matokeo
chanya kwa kuongeza mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi na utendaji kazi
katika chuo hicho.
Kwa namna ya kipee Prof. Kabote
amewaasa wafanyakazi wote kutumia nafasi hiyo ya msimu huu wa sita kushiriki
kikamilifu katika michezo yote na kila mmoja awe na hari ya kufanya mashindano
hayo kuwa ni moja ya tukio katika Maisha yake kama mfanyakazi ikiwa na lengo la
kumsaidia kumuweka sawa kimwili, kiakili na kuboresha mahusiano yake binafsi
katika eneo la kazi.
Katika tukio hilo mara baada ya
ufunguzi Michezo iliyoanza kutimua nyasi za viwanja vya Edward Moringe Sokoine ni
Pamoja na Mpira wa Miguu, Mchezo wa Kuvuta
Kamba na Mpira wa Kikapu kwa wanawake, ambapo mashindano hayo yataendelea mpaka kufikia kilele chake mwezi Octoba.
0 Comments